24Bongo News :
Home » » YANGA YAPIGWA 2-1 KIBISHI UTURUKI

YANGA YAPIGWA 2-1 KIBISHI UTURUKI

Young Africans imepoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Denizlispor FC ya Uturuki kwa mabao 2-1 katika mchezo uliofanyika katika viwanja vya Selen football - Kamelya Complex pembeni kidogo mwa mji wa Antalya.

Young Africans iliuanza mchezo kwa kasi kwa lengo la kusaka bao la mapema zaidi lakini umaliziaji wa washambuliaji Saimon Msuva na Jerson Tegete katika dakika za 7, 15 na 24 uliikosesha mabao ya mapema.

Young Africans ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao kunako dakika ya 35, mfungaji akiwa ni Jerson Tegete akimalizia pasi safi iliyopigwa na Saimon Msuva kufuatia migongeo mizuri ya Haruna Niyonzima na Athuman Idd 'Chuji


Young Africans ileindelea kutawala mchezo kwa kipindi chote cha kwanza na hadi timu zinakwenda mapumziko Young Africans ilikuwa mbele kwa bao 1-0 Kipindi cha pili Denizlispor FC ilifanya mabadiliko ya kikosi chake kuanzai mlinda mlango mpaka washambuliaji wake, lakini mabadiliko hayo bado hayakuweza kuisadia kwani umakii wa walinzi Kabange Twite, Nadir Haroub 'Cannavaro, Kelvin Yondani na Juma Abdul ulikuwa kikwazo kwao kumfikia mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez'.

Dakika ya 78 Denizlispor FC ilijipatia bao lake la kwanza, baada ya mfungaji kupiga shuti lililokwenda moja kwa moja wavuni ili hali walinzi wa Young Africans na mlinda mlango Ally Mustafa 'Barthez' wakisubiri kusikia filimbi ya mamuzi kwani mfungaji kabla ya kufunga alikuwa ameunawa mpira ndani ya eneo la hatari
.
Huku mpira ukiwa katika dakika za mwisho kabla ya kumalizika, mwamuzi wa mchezo ambaye hakuonekana kuwa makini aliwapatia wenyeji Denizlispor FC penati dakika ya 88, penati ambayo ilileta utata kutokana na mwamuzi kupishana na mshika kibendera aliyekuwa ameonyesha kuwa mshabuliaji wa Denizlispor alikuwa amemfanyia madhambi nahodha Nadir Haroub, Denizlispor FC walipiga penati hiyo na kujihesabia bao la pili na la ushindi
.
Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 1- 2 Denizlispor FC.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard