Ikiwa ni siku chache zimepita tangu kuuwawa kwa risasi kwa padre Evarist Mushi huko Zanzibar, watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe na baadae kulichoma moto kanisa la Walokole la Shaloom lililoko Kiyanga kwa Sheha mkoa wa kusini Unguja Zanzibar.
Kamanda wa polisi mkoa wa kusini
Unguja Agustino Ulomi amesema hilo tukio limetokea jana saa tisa na nusu
usiku, ambapo huo moto ulianza kuwaka baada ya vijana watatu
walioonekana karibu na kanisa, baadae kidogo ndio mlinzi akaanza kusikia
mawe yakirushwa juu ya bati.
Baada ya mlinzi kuona hatari ilibidi akajifiche lakini kwa mbali akawa anaona kinachoendelea, moto ukiendelea ndio akampigia simu kiongozi wa kanisa ambae aliwapigia polisi, wakaja wakawa wanashirikiana na wananchi kuuzima japo tayari ulikua umeshaunguza samani mbalimbali za kanisa hilo, kilichosaidia kanisa hilo kutoungua lote ni vifaa imara vilivyotumika kulijenga.
Katika ripoti hii ambayo
imeripotiwa na mwandishi wa habari Cathbert Kajuna wa
kajunason.blogspot.com bado hajakamatwa mtu yeyote mpaka sasa, polisi
wamesema pia wanaanza utaratibu wa ulinzi wa makanisa kutokana na
vitisho vilivyopo sasa hivi.
Hakuna mtu yeyote
aliejeruhiwa katika tukio hilo lililotokea saa tisa usiku wa kuamikia
leo
0 comments:
Post a Comment