24Bongo News :
Home » , » "SISTER" ALIYEFUMANIWA NA MUME WA MTU AHUKUMIWA

"SISTER" ALIYEFUMANIWA NA MUME WA MTU AHUKUMIWA

MAHAKAMA ya Mwanzo mjini hapa,  imemtia hatiani aliyekuwa mtawa wa Shirika la Kitawa la Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga, Sista Yasinta Sindani, kwa kufumaniwa na mume wa mtu na kuamriwa kumlipa fidia ya Sh 700,000 mlalamikaji.  

Katika kesi ya msingi ya madai, mlalamikaji Asteria Mgabo alimtaka Sista Yasinta amlipe Sh milioni 3 baada ya kumfumania na mumewe wa ndoa, Martin Msangawale (39) ambaye pia ni mkazi wa mjini hapa.  

Sista huyo ambaye ni daktari katika Hospitali ya Mkoa wa Rukwa mjini hapa, kwa sasa anaishi nje ya nyumba ya utawa eneo la Kantalamba. 

Katika hati ya awali ya madai, inadaiwa mshitakiwa alifumaniwa na Asteria akiwa na mumewe Msangawale wakiwa kwenye nyumba ya kulala wageni  ijulikanayo kwa jina la Chipa iliyopo eneo la Katandala mjini hapa, Desemba 24  mwaka jana majira ya saa 7 usiku  ikiwa ni siku ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas. 

Akisoma  hukumu  hiyo juzi, hakimu wa  mahakama  hiyo, Jaffar Mkinga alisema kuwa ushahidi uliotolewa na mlalamikaji ulikuwa mzito wenye kuondoa shaka zote  kuwa mdaiwa alitenda kosa hilo tofauti na utetezi  uliotolewa na mdai kuwa ulikuwa dhaifu. 

Awali katika  utetezi wake  mdaiwa  aliiambia mahakama  hiyo kuwa  kwanza alikuwa hajui kuwa Martin alikuwa  mume wa mtu na kukiri mbele ya mahakama hiyo kuwa alimweleza kuwa hana mke hivyo alimwomba amuoe.  

Lakini Hakimu Mkinga alipinga utetezi huo kwa sababu usiku  huo wa mkesha  wa Krismas  mwaka jana, saa saba na robo usiku, mlalamikaji akiongozana na mwenyekiti wa mtaa wakiwa na mashahidi wengine watatu,  walimkuta mdaiwa na Martin wakitoka katika   moja ya vyumba katika nyumba ya kulala  wageni ya Chipa, akasainishwa.  

“Kama hukufahamu kuwa Martin alikuwa  hana  mke ilikuwaje ukakubali kusaini karatasi hiyo ya fumanizi  iliyoandaliwa na mwenyekiti  huyo?” alihoji hakimu, akamhukumu kulipa sh 700,000.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard