24Bongo News :
Home » » SHABIKI AMWANDIKIA ARSENE WENGER BARUA

SHABIKI AMWANDIKIA ARSENE WENGER BARUA



Mpendwa Bwana Wenger.

Nakupenda,tena nakupenda sana.

Kwanini unatutendea hivi sisi mashabiki wa Arsenal kila mahali? Kwanini unawaacha katika gizani nene na hawajui hitimisho la timu yao?

Kwanini mpaka sasa ujanunua mchezaji yeyote katika dirisha hili? Kwa nini mpaka sasa ni nusu wa mwezi January hakuna hata tetesi ya usajili wa mchezaji yeyote?

Kwa nini umekuwa ukidhoofisha timu yetu ya Arsenal kwa miaka kadhaa kwa kuuza wachezaji muhimu huku timu yetu ikihangaika kupigania nafasi ya nne sasa?

Nahisi swali muhimu hapa ni,Una mipango gani na timu ya Arsenal?

Kwa nini hutaki kusikiliza maelfu ya mashabiki wanakupigia makelele kwamba jambo Fulani lilifanyike? Sikiliza hili kundi linalopiga kelele, Mr. Wenger. Kuwaacha mashabiki wa timu hii kwenye giza ni sawa na kuwamwagia maji taratibu kwenye paji la uso. Au ni sawa na kutufanya wote tusikilize nyimbo ya "Friday" wa Rebecca Black kwa kurudiwa kupigwa.

Tafadhari acha. Tufanye wenye furaha. Hicho ndicho nachoomba.

Ungeelekeza nguvu kwenye kuimarisha timu na si kuchezesha wachezaji walewale. Kwani bado hujagundua kwamba Arsenal bado inahangaika,na hasa hata katika mechi ya kipigo cha Manchester City ?

Kwani kusema kwamba utanunua wachezaji wenye ubora kwenye vyombo vya habari ni muhimu?Na hilo ndo kazi yako unayopaswa kuifanya. Na ndo tuchotegemea kutoka katika timu yetu. Ila kwa mara nyinine tena ukawaleta, Gervinho, Andre Santos and Park Chu-Young. Hivyo siwezi tena kukuamini usemacho.

Kwa nini tunaendelea kutetea gharama kubwa ya tiketi za mechi wakati timu iko mbali kabisa kuweza kupigania ubingwa wa Ligi kuu? Kwa nini gharama zisiendane na matokeo uwanjani?

Bwana Wenger, Ninapenda useme wazi tatizo ni nini klabuni. Natamani nione ukipatwa na hasira ya mafanakio. Nataka nione unafanya kila namna kuhakikisha Arsenal inashiriki Ligi ya Mabingwa. Nataka kuona uhalisi wa ubinadamu wako.

Kama mshabiki, Sijali kwamba klabu inatengebeza faida au hapana. Hata wewe pia usijali

Nakupenda, Bwana Wenger. Bado wewe ni mtu sahihi wa kuongoza klabu yetu.Lakini kila siku inayopita bila kusaini mchezaji,inatufanya mimi na mashabiki wengine tuwe na wasiwasi sana.

Tafadhari fanya kitu sasa. Tafadhari

Wako

Shabiki-The Gunners

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

1 comments:

Anonymous said...

Huyu Kocha anazingua sana khaaa

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard