MALI YAITANDIKA GHANA MSHINDI WA TATU
TIMU ya taifa ya Mali jana imeifunga
mabao Ghana 3-1 na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la
Mataifa ya Afrika, wakiipiku Black Stars kwa mwaka wa pili mfululizo
kwenye mashindano haya.
Mshambuliaji Mahamadou Samassa alifunga
bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 21, Nahodha Seydou Keita akafunga la
pili dakika ya 48 na Sigamary Diarra akahitimisha karamu hiyo ya mabao.
Kwadwo Asamoah aliifungia Ghana bao la
kufutia machozi dakika ya 82. Mshambuliaji wa Ghana, Wakaso Mubarak
alikosa penalti mapema kipindi cha pili.
Mwaka jana, Mali iliifunga Ghana 2-0
katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu. Waliingia kwenye michuano ya
mwaka huu wachezaji wakisema wamedhamiria kufanya vizuri ili kuwapa
faraja mashabiki wao kwa vurugu za kisiasa zinazoendelea nyumbani kwao.
Kipigo cha jana ni pigo lingine kwa Ghana, baada ya kuingia Nusu Fainali kwa mara ya nne mfululizo bila kuingia Fainali.
Ghana iliingia kuwania nafasi ya tatu
baada ya kutolewa na Burkina Faso kwa mikwaju ya penalti kwenye Nusu
Fainali. Black Stars walitwaa taji la mwisho la Mataifa ya Afrika mwaka
1982.
Kikosi cha Mali:
Soumaila
Diakite, Diawara, Salif Coulibaly, Adama Coulibaly, Tamboura, Ousmane
Coulibaly, Kalilou Traore, Mahamane Traore, Mahamadou Samassa (Sigamary
Diarra 78), Keita, Diabate.
Benchi: Mamadou Samassa, N'Diaye, Wague, Maiga, Sissoko, Idrissa Coulibaly, Cheick Diarra, Yatabare, Sow, Samba Diakite, Yirango.
Kadi ya njano: Tamboura.
Wafungaji wa mabao: Mahamadou Samassa 21, Keita 48, Sigamary Diarra 90.
Kikosi cha Ghana:
Dauda, Richard Boateng, Vorsah, Boye (Mensah 46), Afful, Wakaso,Awal, Asamoah, Asante, Atsu (Adomah 70), Gyan (Clottey 75).
Benchi: Agyei, Pantsil, Annan, Agyemang-Badu, Derek Boateng, Rabiu, Akaminko, Boakye, Kwarasey.Kadi za njano: Wakaso, Vorsah, Asante.Mfungaji wa bao: Asamoah dk82.
Mahudhurio: 6,000
Refa: Eric Otogo-Castane (Gabon)
0 comments:
Post a Comment