24Bongo News :
Home » » MFANYABIASHARA AMPIGA RISASI POLISI,AJIUA

MFANYABIASHARA AMPIGA RISASI POLISI,AJIUA

   MFANYABIASHARA, Yemuga Fugungu (48), mkazi wa wilayani Bukombe, mkoani Geita, amejiua kwa kujipiga risasi baada ya kudhani amemuua askari wa kituo cha Runzewe, Fortunatus Beatus.

 

 Kamanda wa polisi mkoani Geita, ACP Leonard Paul, ameiambia Tanzania Daima kwa njia ya simu kuwa tukio la mfanyabiashara huyo kujiua lilitokea juzi majira ya saa 2.30 usiku.

 

Alisema awali gari la mfanyabiashara huyo lilikamatwa na askari wa doria waliokuwa katika eneo la Nyantare kwenye barabara kuu ya Runzewe na Nakanyaki likiwa limebeba kokoto zinazodaiwa kuwa ni za wizi.

 

Kamanda Paul alisema baada ya gari hilo kukamatwa mfanyabiashara huyo aliyeonekana amelewa alianza kuwafokea askari kwa kuwataka waliachie gari lake hali iliyozua mabishano baina yao.

 

Alisema katika mabishano hayo Fugungu alitoa bastola na kuwarushia risasi askari na kusababisha majeraha kwa mmoja wa askari waliokuwa karibu na tukio hilo na kujeruhiwa tumboni na pajani kisha mfanyabiashara huyo akakimbia kutoka eneo la tukio.

 

Aliongeza kuwa baada ya kufanikiwa kukimbia mfanyabiashara huyo aliingia katika nyumba ya jirani ya mwanajeshi wa eneo hilo na kuwalazimisha watu waliokuwa ndani wampatie mavazi ya askari wa jeshi la wananchi na kisha kutokomea nayo nyumbani kwake.

 

“Yule bwana alikuwa amelewa na alipoona ameshamjeruhi askari akajua amemuua sasa akaenda kwenye nyumba ya jirani ambapo kulikuwa na mwanajeshi aliyekuwa likizo na kulazimisha apewe mavazi ya kijeshi na kutokomea nayo,” alisema Paul.

 

Alibainisha kuwa baada ya mfanyabiashara huyo kuchukua mavazi hayo ya kijeshi alielekea nyumbani kwake ambapo polisi walimfuata kwa lengo la kumkamata.

 

Alisema wakati askari wakiwa katika harakati za kumdhibiti Fugungu aliendelea kuonyesha ukaidi hali iliyowalazimu askari warushe bomu la machozi katika nyumba aliyojifungia.

“Liliporushwa bomu la machozi yule bwana aliamua kujilipua kwa risasi nadhani alijua kuwa ameshamuua askari wetu kutokana na kumpiga risasi tumboni na mapajani,” alisema Kamanda Paul.

 

Alisema mwili wa mfanyabiashara huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti kwenye Hospitali ya Bukombe.

source:freemedia 

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard