Kehinde Adesamuye, 39, mkazi wa
Lagos, Nigeria anadaiwa kumchoma kwa moto wa petroli hivi karibuni mkewe
Janet Udegba, 35, katika Mtaa wa Ikotun jijini Lagos baada ya kuwa na
hasira kutokana na kuhisi kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na mwanamume
mwingine.
Janet alisema wakati wa tukio hilo, alikuwa katika eneo lake la biashara
akiuza vyakula kabla ya Kehinde kufika hapo usiku huo na kumwagia
petroli mgongoni kisha kuwasha moto kwa kutumia kibiriti.
Hata hivyo, alisema Wanigeria hawatamwachia huru Kehinde kutokana na kile alichokifanya. Akisimulia mgogoro wao, anasema:
“Mume wangu amekuwa na wivu daima. Amekuwa na tabia ya kunipiga kila
wakati. Nimejaribu mara nyingi kuachana naye lakini huwa ananitishia
kuwa lazima atanidhuru. Niliendelea kuishi naye kwa kuwa nilikuwa na
hofu ya maisha yangu, aliwahi kuniambia kuwa sitaweza kutoroka hata siku
moja.
“Serikali lazima ihakikishe kuwa Kehinde analipa kwa kile
alichonifanyia. Mimi ni yatima, ninafanya biashara ya vyakula ili
niishi. Sasa nimetumia pesa zangu zote kwa ajili ya matibabu. Kwa kweli
kwa sasa nahitaji msaada,” alisema mama huyo huku akitokwa machozi.
Kehinde alijaribu kutuma rafiki zake ili wamwombee msamaha kwa Janet lakini alikataa. Mtuhumiwa huyo anashikiliwa na polisi kwa ajili ya kujibu mashtaka yanayomkabili.
0 comments:
Post a Comment