Mkuu wa
Jeshi la Polisi Nchini Said Mwema akimkabidhi pikipiki Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar Es Salaam, Naibu Kamishna wa Polisi Suleiman Kova
kama ishara ya kukabidhiwa Makamanda wote Tanzania bara na Visiwani
ambapo jumla ya Pikipiki 564 zimekabidhiwa kwa ajili ya kuzuia uhalifu
kwa lengo la matumizi ya Wakaguzi Tarafa wa Polisi Tanzania bara na
Majimbo yote ya Zanzibar, program za Safiri Salama na Usalama wetu
kwanza.
Makabidhiano
hayo yamefanyika katika makao makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es
salaam na kuhudhuriwa na Makamanda na maafisa mbalimbali wa jeshi hilo.