24Bongo News :
Home » » KICHANGA CHAKUTWA KIMETUPWA IRINGA

KICHANGA CHAKUTWA KIMETUPWA IRINGA

 
 
Mtoto wa jinsia ya kike anayekadiriwa kuwa na umri wa siku moja amekutwa ametelekezwa pembeni ya mto karibu na chuo kikuu cha Tumaini Iringa.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa kitendo hicho ni cha kinyama zaidi katika eneo hilo na hii inaonesha jinsi gani watu wasivyo na utu.

"Inavyoonekana mtu huyu alijifungua halafu akamtupa mtoto huyu, hii ni ajabu sana kwa mtu kubeba mimba miezi tisa halafu kuamua kutupa kiumbe kisicho na hatia" alisema kijana huyo aliyefahamika kwa jina moja Rajabu

Kwa mujibu wa kijana aliyeona mwili huo alisema alikuwa anaelekea shambani na ndipo alipoamua kupitia sehemu ambayo huwa anaficha jembe na kuona kiumbe huyo akiwa ametelekezwa huku akiwa amekwisha kufa.

"Inawezekana mtu huyu alimtupa mtoto huyu usiku kwani jana wakati naficha jembe hapakuwa na kitu chochote "alisema kijana huyo.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard