![]() |
Tundaman |
Msanii maarufu wa kundi la TIP TOP,Tundaman amekana story zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya blogs kwamba ameporwa Mil 7 na jimama. Habari hizo ni za uzushi na zimemkera sana anashangaa kwanini watu wanavumisha habari hizo?
Alisema alipokuwa akizungumza na Dj Choka
"Hizi habari si za kweli Choka, unajua mambo mengine hata mzazi wako anaposikia habari zakuibiwa hela sijui na jimama wakati yeye anashida na hela anakuwa hala amani tena na wewe kwasababu unaweza kukuta alikuomba kiasi kidogo lakini wewe ulimpiga chenga ili ujipange zaidi halafu mtu anakuja kusema nimeibiwa Mil 7 na jimama wakati hata hizo hela sina kwa wakati mmoja"
Tundaman amewaomba mashabiki wake wasichukulie habari hizo kama zilizovyo kwa maana ni uzushi mtupu kwa wanaotaka kumwalibia jina lake.