Jeshi la Polisi limevalia njuga sakata la
biashara ya uuzwaji wa wasichana wanaosafirishwa kwenda nchi za nje.
Tayari jeshi hilo limeshawaondoa kazini
askari wa kikosi cha bandari waliokuwa wakibariki biashara hiyo kutoka bandari
ya Dar es Salaam kwenda Zanzibar kisha baadaye kupelekwa nchi za Urabuni Kuliko
soko hilo
Hata hivyo wenyeviti wa mtaa waliohusika katika kuwapatia barua kutoka katika mkitaa yao wapo katika hatua za kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kughushi barua ili wasichana wao watambuloike wanatoka kwenye mitaa yao
Wasichana hao imebainika kutokea mikoa tofauti nchini kufikia Dar es salaam wka mawakala kisha kupelekwa Zanzibar na baadae kupelekwa uarabuni
Biashara hiyo ilianza mwishoni mwaka jana na januari kushika kasi zaidi ambapo imebainika mabinti hao haswa kutokea mikoa ya Pwani, Tanga, Lindi, Tabora Ruvuma
Imebainika Mawakala hao wakifanikiwa kuwafikisha wanakohitajika hujinyakulia Dola za KiMarekani 5,000 sawa na Sh. milioni 8 kwa kila mtoto na wazazi wa watoto hao hudanganywa kwa kupewa kiasi kidogo cha fedha
Katika uchunguzi uliofanywa na mtandao huu uliotembelea vijiji kadhaa katika mikoa ya Pwani na kusini imegundua ni kweli kuna baadhi ya wazazi hutoa mabinti zao na watoto wa kiume kwa kuahidiwa kiasi cha fedha kwa kuambiwa watoto hao wametafutiwa kazi na wawili kati ya walioyohojiwa wamethibitisha kupatiwa fedha kiasi kisichozidi shilingi laki tano za kitanzania
0 comments:
Post a Comment