24Bongo News :
Home » » KANISA LA AJABU JIPYA LAIBUKA DAR ES SALAAM

KANISA LA AJABU JIPYA LAIBUKA DAR ES SALAAM



Kanisa hilo ambalo linajulikana kwa jina la The Pool of Siloam lililoko Mbezi- Makonde, Kinondoni, Dar es Salaam linafanya ibada zake Jumanne badala ya Jumapili wakiamini ndivyo Neno la Mungu linavyotaka.

Jambo lingine ambalo linachagiza u-ajabu wa kanisa hio ni kupinga jina la Biblia Takatifu. Muumini mgeni anayefika kwenye kanisa hilo hulazimika kukabidhi Biblia yake kwa uongozi ambapo wao hutoa ‘kava’ ya nje yenye jina la Biblia na kuweka kava nyeupe yenye maandishi ya Kitabu Cha Bwana.

Kama vile hayo hayatoshi, kanisa hilo linaamini siku za mwezi ni 28 na si 29, 30 au 31. Wanasema Mungu alipanga hivyo na ndiyo maana aliwapa hata wanawake mzunguko wa siku 28 kuingia katika hedhi.

“Kinachotuingiza kwenye majira halisi ya Mungu ni kufuta tarehe 29, 30 na 31 za Julius Kaisari katika kila mwezi wa kalenda ya Gregori kwa mamlaka ya Mungu wa Majeshi ili kuondoa uovu ulioambatana na tarehe hizo za ziada kwenye miezi 12 ya mwaka,” alisema muumini mmoja kanisani hapo.

Uchunguzi unaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo lilichapisha kitabu ambacho kinaonesha kuwa mwanzo wa mwaka si Januari bali ni Machi (wao huita Abib au Aviv). Na mwisho wa mwaka si Desemba, bali ni Februari (wao huita Adari).

Kwa ugunduzi wao huo, kuanzia mwaka 2008 kanisa hilo hawafanyi ibada ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Bwana Yesu Desemba 25, yaani Krismasi kama madhehebu mengine ya Kikristo kwa vile wanaaminiYesu alizaliwa Februari 28.

Uwazi lilipata nafasi ya kupenya hadi ndani ya kanisa hilo ambalo limejengwa kisasa na kukutana na kiongozi mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Daudi Elia ambaye alisema kuwa makanisa mengi hayafanyi kama ambavyo Mungu ameagiza.Aidha, Daudi alimtaja kiongozi mkuu wa kanisa hilo kuwa ni Mchungaji Elia Amu wa Pili Mungu wa Majeshi Mtume na Nabii wa kizazi cha nne na akabainisha kuwa, awali alikuwa akifanya kazi Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) kama mhandisi.

“Aliacha kazi ya uhandisi na kuanza kumtumikia Mungu wa kweli kuanzia mwaka 2003, kazi ambayo amekuwa akiifanya hadi sasa ambapo kanisa limesimama na kuenea Tanzania nzima na duniani,” alisema Daudi.

Aliongeza kuwa, Mungu alimwambia nia ya kumteua afanye kazi za kiroho ni kuvunja misingi mibovu ya kumuabudu na kuiweka inayofaa.
Mchungaji huyo ambaye alikuwa akiongea kwa niaba ya kiongozi mkuu, alisema kanisa hilo limekuwa na maagizo ya kweli ambayo Mungu aliagiza yafanyike.
Kiongozi huyo akizungumzia namna ya kujiunga na kanisa hilo alisema kuwa, sharti la kwanza ni mtu kubadili jina lake la awali na kupewa lingine ambalo ni matakwa ya Mungu kisha kubatizwa upya.

Alisema kanisa hilo halikubaliani na mambo ya dunia kama vile kuwa na Siku ya Kifua Kikuu, Siku ya Ukoma, Siku ya Ukimwi na kadhalika kwa vile kufanya hivyo ni kwenda kinyume na ufalme wa Mungu.Hata hivyo, baadhi ya waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kiluteri Tanzania (KKKT) wanaoishi jirani na kanisa hilo walipohojiwa kuhusiana na nyumba hiyo ya ibada walisema wana wasiwasi na nguvu za kishirikina ndiyo zinaratibu mwenendo wao.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard