MSANII
wa nyimbo za muziki wa bongo fleva anayefahamika kwa jina la Baby
Madaha amewashukia baadhi ya wasanii wa kike nchini wanaojihusisha na
maswala ya ngono na wanaume wenye umri mdogo maarufu kwa jina la
'Kijibwa' kuwa ni hali ya kukata tamaa na ushamba ndio unaochangia
kufanya kitendo hiko
Akizungumza jijini Dar es Salaam Msanii huyo
alisema kuwa anashangazwa na baadhi ya wasanii hususani wa kike
kujihusisha na maswala ya ngono na wavulana wenye umri mdogo huku
wakitumia jina la 'kijibwa' kwa ajili ya kukidhi matakwa yao ya kingono
Alieleza
kuwa hali ya kukata tamaa ndio chanzo kinachopelekea baadhi ya wasanii
hao kujihusisha na maswala ya ngono na vijana wadogo huku wakijipa moyo
kuwa wanatafuta faraja wakiwa na vijana hao
"Unajua hao wasichana
wanaonekana kukata tamaa kwa kukosa mwanaume wanaolingana kiumri ndio
maana ajimchukua mtoto mdogo na kumuhudumia kila kitu na ndipo hapo jina
la 'kijibwa' linapotumika kwa kumfananisha mvulana huyo na mbwa
unayemuudumia kila kitu huku kazi yake kubwa inakuwa ni kumlinda tu "
aliongezea kuwa
"Kwa sababu mvulana huyo anapewa kila kitu
ikiwemo kununuliwa hadi nguo yeye anakuwa na kazi moja tu hivyo hapo
hamna mapenzi zaidi ya utumwa na kumsababisha mvulana huyo kukosa uhuru
wa kuwa na maamuzi ya mambo yake binafsi" alisema Madaha
Kutokana
na hicho kitendo Madaha alikiita ni ushamba kwa kuwa na mahusiano
ambayo hayana msingi wowote ule na si kwa ajili ya mtazamo wa maisha
hivyo mahusiano hayo hayaendana na mazingira ya nchi na kusababisha
kudharaulika kwenye jamii inayomzunguka
Alitoa wito kwa wasichana
hao wanaojihusisha na maswala hayo kuwa wanachotakiwa ni kujiamini na
kujipanga upya kwa ajili ya kupambana na maisha na kutoyaogopa maisha
hivyo wanachotakiwa ni kujipanga upya.