MATUKIO KATIKA PICHA
Akizungumzia kasumba ya watanzania wengi kutopenda kusoma vitabu na jinsi alivyokabiliana nayo Nancy anasema, “nilimshirikisha mchoraji mzuri sana kwasababu nilitaka kumvutia mtu kwa wepesi kwanza kiwe kifupi, yaani kidogo. Ni kitabu ambacho unaweza kukipitia ndani ya dakika tano. Kuna picha nyingi lakini meseji yake ni nzito sana.”
Kwa upande wake Profesa Mwaikambo(74), ambaye mwaka huu ubalozi wa Marekani ulimtunuku tuzo ya haki ya Dk Martin Luther King amempongeza Nancy kwa kuandika kitabu hicho na kusema kuwa watoto wengi hasa wenye kuanzia umri wa miaka mitatu wataweza kukifurahiia kwa kuangalia picha tu.