24Bongo News :
Home » , » PAZIA LA LIGI KUU VODACOM LAFUNGULIWA BAADA YA TIMU SHIRIKI KUKABIDHIWA VIFAA

PAZIA LA LIGI KUU VODACOM LAFUNGULIWA BAADA YA TIMU SHIRIKI KUKABIDHIWA VIFAA

Mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL), Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, jana ilivikabidhi vilabu 16 vitakavyoshiriki ligi hiyo msimu huu kwa kuzipatia vifaa vipya vya michezo vyenye thamani ya Sh. milioni 490 kwa ajili ya msimu huu.
Vifaa hivyo vimekabidhiwa jana katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam .Mkuu wa idara ya  Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Kelvin Twisa, akisema kutolewa kwa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa matakwa ya kimkataba kati yao na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kuhakikisha ligi hiyo inaendeshwa vizuri
 

“Kwa niaba ya Vodacom Tanzania, ninazitakia kila la kheri timu zote 16 zinazoshiriki VPL msimu huu. Timu bora na ishinde,” amesema Twissa.

Vifaa vilivyokabidhiwa kwa wawakilishi wa klabu zote 16 ni pamoja na jezi za mechi, jezi za mazoezi, mipira, viatu, soksi, vilinda ugoko, nguo za kawaida kwa ajili ya wachezaji na maofisa wa klabu, glavu na vitendea kazi vya waamuzi.
 
 
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu nchini (TPLB), Boniface Wambura, aliushukuru uongozi wa Vodacom Tanzania kwa kuongeza mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya Sh. bilioni 6.7 kuendelea kuidhamini ligi hiyo.Wambura aliahidi kuwa bodi hiyo itashirikiana na TFF kuhakikisha ligi inachezwa bila upendeleo kwa baadhi ya timu. 

“Timu zimeongezeka kutoka 14 hadi 16, hivyo tutakuwa na mechi 240 msimu huu. Tumejipanga kuhakikisha tunakuwa na ligi bora kuliko msimu uliopita,” amesema.
 

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard