Masuala yote ya usajili ya wachezaji ndani ya hii timu chini ya Van gaal ndicho kinachofuata sasa..Ni mwaka mmoja sasa toka Van Gaal atue Manchester United na gharama za usajili mpaka sasa zinakaribia paundi milioni 170.
![]() |
Kocha wa Manchester United ..Lousi Van Gaal |
Hii ni uwekezaji mkubwa sasa ndani ya Manchester United na kinachofuata sasa ni kupigania ubigwa.Kocha huyo ameitoa Manchester United nafasi ya saba na kuirudisha kushirikia michuano mikubwa ya Mabingwa wa Ulaya na tayari ina wachezaji wazuri kikosini.Ikitokea wakashindwa kuingia nafasi tatu za juu hayatakuwa mafaniko ndani ya klabu.Shinikizo ni kubwa kwa Louis Van Gaal kuweza kufanikisha hayo yote.
Bado tumeona Manchester United wakijaribu kutupa karata ya mwisho kwenye usajili siku ya mwisho(Deadline Day).Ni vigumu kuhamini usajili wa namna hiyo nyakati za Sir Alex na David Gill.Ilikuwa ni aibu sana.Usajili wa Anthony Martial ni usajili mzuri ikiwa utaleta matunda haswa kwa umri wake na uzoefu mdogo alionao na kwa gharama kubwa waliotumia.Mchezaji huyu anafananishwa na Thiery Henry mpya huko Ufaransa.
![]() |
Anthony Martial baada ya kumaliza usajili kutua Manchester United. |
Van Gaal anapenda mchezaji mwenye spidi na ambae anakaa na mpira..alikuwa na Arjen Robben pale Bayern Munich ,akajaribu na kushindwa kumfanya Angel Di Maria kuwa mchezaji wa namna hiyo Manchester United.Anthony Martial anaweza kwa staili anayopenda Van Gaal lakini ni risk sana kwa kijana mdogo ambae ana uzoefu wa kutosha kutoa matokeo ya haraka.
Van Gaal akufikiria chochote juu ya kumuuza Di Maria kwa hasara baada ya kuwa amemnunua mwaka mmoja tu na kwa namna Di Maria na Falcao walivyoshindwa kung'ara kwenye timu yake inamuondolea credits Van Gaal.
Tatizo kuwa kwa Van Gaal ni Man Management.Mfano:Sakata la De Gea ..Hili lilikuwa wazi ..kama hakukuwa na ofa yoyote kutoka Real Madrid mpaka siku ya mwisho kwa nini hakuwa akimcheza kipa huyo?Kumweka na kikosi cha akiba isingeweza kumbadilisha mawazo yya kubaki klabuni hapo.
Baada ya mapumziko mafupi ya mechi za taifa suala hili litakuwa limepoa lakini si kwa De Gea ambae katika kipindi hicho chote amekua very professional na pia atacheza akirudi.Unaweza pia ukajiuliza kama jinsi Van Gaal alivyowatreat De Gea na mhispaniola mwenzake Victoer Valdes kulikuwa na msukumo wa Pedro kuhamua kwenda Chelsea...labda!
Huenda hatujui kinachoendelea ndani ya chumba cha kubadilishia nguo klabuni hapo ila inapokea kila mchezaji ametoka klabuni hapoa akasema kilichokuwa kinaendelea hatuna budi kujiuliza maswali zaidi.Wachezaji watamheshimu kocha ambae atakuwa na msimamo wa maamuzi yake na kuyaelezea maamuzi .
Ilinishangaza sana mwaka jana Van Gaal kusema mbele ya waandashi kwamba hamchezeshi Luk Shaw kwa sababu hayuko fiti na sasa ana matatizo na Rojo,Je unafikiria Adnun Januzaj atafikiria nini?Mwanzo ilionekana kama atapewa nafasi kikosini ghafla kapelekwa Ujerumani kwa mkopo..
Kinachowauma mashabiki wa United ni namna wahitimu wa soka ndani ya shule yao wanavyopukutika na nguvu ya Manchester ilikuwa ikijengwa na shule yao.Kikosi cha ushindi cha mwisho cha akina Danny Welbeck,Darren Fletcher,Tom Clevery na Jonny Evans kimeshaondolewa na kuna hisia kwamba Manchester inapoteza uhalisia wake.
Majina makubwa yanakuja na kuondoka klabuni..Ukweli ni kwamba Van Gaal anapoteza ile hali na uhalisia wa Manchester United tulioizoea na ile aina ya uchezaji wao ambao ni maarufu nchini umepotea kwani sasa wanamiliki mpira vizuri lakini hawashambulii kama zamani.
Kwa mtazamo wa haraka haraka unaweza kugundua kwamba Manchester ya sasa inataka kushindana na majirani zao ambao wana kila wachezaji wazuri wawili kwenye kila nafasi uwanjani.Manchester United bado ina upungufu wa wachezaji wawili..watatu kikosini lakini kwa kuwa gharama ambazo Van Gaal ameshatumia kwa usajili ni vema ikazaa matunda kwa namna yoyote ile.
ALLL THE BEST.
By JR