- Baada ya maandalizi nchini Uturuki sasa iko kamili kuivaa Nigeria
- Vicent Enyeama ajitoa Kikosini kwa sababu za kifamilia
- Mtihani wa kwanza wa Kocha Sunday Oliseh wa Nigeria
- Taifa Stars haijawahi kuifunga Nigeria
- Samatta,Mrisho Ngasa na Ulimwengu watabiriwa kuimaliza Nigeria
Kikosi cha Nigeria kinachoundwa na nyota wengi wanaosakata soka la kulipwa nchini Ulaya na kwingineko watakuwa na kazi ngumu ya kuizuia Taifa Stars yenye hali na motisha mpya mbele ya mashabiki.
Timu zote mbili zinakutana ikiwa ni baada ya kufanyiko mabadiliko ya ufundi .Upande wa Nigeria ,Kocha Sunday Oliseh ambae amechukua mikoba ya Kocha Stephen Keshi atakuwa ana kibarua kigumu ugenini kuiwezesha timu hiyo inayosukwa upya kuondoka na ushindi huku ikiwa imeshampoteza kipa na mchezai wake mzoefu Vicent Enyeama kwa sababu za kifamilia.Kipa huyo atakuwa ni pengo kubwa kwa Nigeria hasa ukizingatiwa uzoefu wake kwa mechi za kitaifa.
Huku Taifa Stars ikiwa chini ya benchi jipya la Ufundi likiongozwa na Mkwasa ,ni wazi kwamba ushindi pekee ndo lengo la Taifa Stars kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kufuzu fainali za Afrika 2017.Nyota wa kutegemewa wa Stars Mbwana Samatta anaechezea TP Mazembe ataongoza mashambulizi huku akisaidia na Mrisho Ngasa,Thomas Ulimwengu na John Bocco.
Ni matumaini yetu watanzania tunaondoka na ushindi kwa kuipa nguvu timu yetu ya Taifa Stars kesho.Tukutane UWANJA WA TAIFA.ALL THE BEST TAIFA STARS