24Bongo News :
Home » , » UHOLANZI YACHAPWA NYUMBANI KWA MARA YA KWANZA...KIBARUA KIGUMU KUFUZU

UHOLANZI YACHAPWA NYUMBANI KWA MARA YA KWANZA...KIBARUA KIGUMU KUFUZU

  • Beki wa Uholanzi Bruno Martins alambwa nyekundu mapema 
  • Glyfi Sigurdsson afunga goli pekee la mchezo huo kwa mkwaju wa penati
  • Kwa mara ya kwanza Uholanzi kupoteza mechi ya kufuzu nyumbani
Timu ya Iceland sasa imebakiza hatua chache kuweza kufuzu fainali za Ulaya nchini Ufaransa baada ya kuwashangaza wenyeji Uholanzi kwenye uwanja wao wa nyumbani.
 
Tukio la penati lilozaa goli pekee la mchezo

Refa aliizawadia Iceland penati yenye utata baada ya beki Van De Wiel kumchezea rafu mchezaji wa Iceland Birkir Bjarnason wakati akijaribu kucheza mpira.Baadae ilionekana wazi Van De Wiel alicheza mpira na haikuwa penati halali.

Glyfi Sigurdsson aliuweka mpira wavuni kwa mkwaju safi wa penati uliomshinda kipa Jasper Cillessen kuipa goli pekee la mchezo huo na kufufua matumaini ya Iceland kufuzu mashindano makubwa katika historia ya nchi hiyo.

Moja ya siku mbaya kwa Uholanzi pale beki Bruno Martins alipotolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kuonekana kumwangusha mchezaji wa Iceland Kolbein Sigthorsson  ambao wote kwa pamoja walianguka chini.

 Kocha mwa Iceland alisema.."Tunaendelea kwenda juu,haya ni mafanikio makubwa sana kwenye mpira wa miguu kwetu"

 Blind nae alisema "Timu ilijipanga vizuri ilicheza kwa umakini na ilikuwa vigumu kupenya ngome yao.Tukio la Bruno ilikuwa ni chanzo cha kupoteza mechi kwani Bruno hakuwa amefanya maamuzi sahihi."
 

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard