24Bongo News :
Home » » HATIMAYE LADY JAYDEE AMALIZA SAFARI YA MLIMANI

HATIMAYE LADY JAYDEE AMALIZA SAFARI YA MLIMANI



Msanii Lady Jay Dee,mumewe Gadner na mpiga picha wao Justine wakimsikiliza kwa makini mhifadhi mkuu wa Mlima Kilimanjaro Erastus Lufunguro.

Mhifadhi mkuu wa mlima Kilimanjaro Erastus Lufungulo akimuongoza msanii Lady Jay Dee mara baada ya kushuka kutoka mlima Kilimanjaro,

 Msanii wa muziki Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee akiwa ameshikwa mikono kusaidiwa kushuka kutoka mlima Kilimanjaro aliko panda Jaanuary 8 mwaka huu na mumewe Gadner G Habash kwa lengo la kutangaza utalii wa ndani.



Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura maarufu kwa jina la Lady Jay Dee, juzi alifanikiwa kukamilisha ziara yake ya siku sita ya kupanda mlima Kilimanjaro, ikiwa na lengo la kutangaza mlima huo na kujionea upekee wa kivutio hicho.
Katika ziara hiyo iliyodhaminiwa na shirika la hifadhi za taifa nchini (TANAPA), msanii huyo aliyeambatana na mumewe ambaye ndiye anesimamia kazi zake, Gadna Habash, waliwasili kwenye lango kuu la Marangu saa 12 jioni na kupokelewa na mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro(KINAPA), Erastus Lufungulo.

Msafara wa Jay Dee ulianza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro Januari 8 na kufanikiwa kufika katika kilele chake chenye urefu wa mita 5895 kutoka usawa wa bahari.
Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari mara baada ya kushuka mlimani, Jay Dee, alisema ziara hiyo imetoa mafunzo makubwa kwao na wakatoa wito kwa wasanii, waandishi wa habari na watangazaji nchini, kutembelea vivutio hivyo ili kufahamu yale wanayozungumza kuhusu hifadhi hizo.

“Ziara hii imenipa mwanga kama msanii, nimejifunza mengi na niwakumbushe tu wasanii wenzangu kuchukulia zoezi la kupanda la kupanda mlima Kilimanjaro kama moja ya majukumu na wajibu wao kama wananchi wa taifa hili,” alisema Jide.

Kwa upande wake mhifadhi wa KINAPA Lufungulo ametoa rai kwa wadau wote hasa wananchi wa kawaida kushiriki kupanda mlima huo, kwa lengo la kukuza utalii wa ndani.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard