24Bongo News :
Home » » SIMBA NA AZAMA HAPATOSHI LEO USIKU KOMBE LA MAPINDUZI

SIMBA NA AZAMA HAPATOSHI LEO USIKU KOMBE LA MAPINDUZI

CHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimefanya marekebisho ya ratiba ya michuano ya Kombe la Mapinduzi na sasa Simba SC itamenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya kwanza leo kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Awali, leo ilikuwa Tusker FC icheze na Miembeni kwenye Uwanja huo, lakini sasa timu hizo zitamenyana kesho katika Nusu Fainali ya pili. Mchezo huo utakuwa ni marudio ya Nusu Fainali ya mwaka jana, ambayo Azam FC waliitoa Simba SC kwa kuichapa mabao 2-1.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali, amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali kuliko Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali. Kuelekea mchezo wa kesho, Kocha wa Miembeni, Salum Bausi amesema hawahofii Tusker na watawaonyesha kwamba mpira ni zaidi yua nguvu Nahodha wa Tusker, Joseph Shikokoti amesema kwamba haoni timu ya kuwazuia kutwaa Kombe la Mapinduzi. Shikokoti aliyewahi kuchezea Yanga alisema kwamba anafahamu Simba na

Azam ni wazuri na anajua mojawapo watakutana nayo fainali, lakini amesistiza hakuna kati yao inayoweza kuwazuia wasitwae Kombe. “Hili Kombe letu, tumeona uwezo wa timu zote, hata Simba na Azam ni wazuri, lakini tutawafunga wote tukikutana nao, hawana uwezo wa kutuzuia,”alisema Shikokoti.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard