Sehemu ya ukaaji wa mashabiki 3000 kwa tiketi takribani 3000, ambapo gharama ya siti moja ni £ 62 kwa mtu mzima hazikuuzwa. Kama hali hiyo klabu imeirejeshea Arsenal tiketi hizo ili iweze kuziuza kwa mashabiki wake
Mchezo wa Manchester City na Arsenal ni mchezo wa daraja A hivyo tiketi zinauzwa bei sana kwa £ 62 kwa watu wazima, £ 23.50 kwa chini ya miaka 16, na £ 26.50 kwa zaidi ya miaka -65. Kwa hali halisi ya mashabiki wa City bei hiyo si ya kawaida, wameshindwa kuuza karibu moja ya theluthi ya tiketi hizo.
Kwa mechi nyingine za daraja A, Tottenham Hotspur na Chelsea wote waliuza tiketi 3000 msimu huu kwa bei hiyo hiyo.
Msimu uliopita, City waliongeza idadi ya tiketi za nje kufikia 5200 kwa bei ya £ 20 na £ 10 kwa ajili ya Kombe la Carling robo-fainali katika uwanja wa Emirates.