Kupitia
segment ya U Heard ya XXL Clouds FM na Soudy Brown, mwimbaji Diamond
Platnums ambae aliongoza kwa kuwa msanii wa bongo alieandikwa sana
kwenye internet mwaka 2012 amethibitisha kumnunulia mkoko mama watoto
wake mtarajiwa.
Soudy Brown alimuuliza kuhusu fununu za kutumia
Milioni 15 kununua gari la mke wake mtarajiwa mtangazaji Penny ambae kwa
sasa ni mjamzito.
Diamond amekiri kwamba ni kweli kamnunulia
Penny gari kwa sababu anaelekea kuwa mama watoto ambapo namkariri
akisema “nilimuuliza gari gani anapenda, nimemuagizia iko njiani inakuja
kwa hiyo sasa hivi anatumia la muda wakati akisubiria gari lake”
Alipoulizwa
kuhusu kumuoa na kama mtoto atazaliwa nje ya ndoa, Diamond amejibu
“siwezi kusema lini ila Mwenyenzi Mungu ndio anajua inaweza ikawa harusi
ila kuna time inafika inabidi utulie, siwezi kusema chochote kwa sababu
inawezekana mtoto akazaliwa ndani ya ndoa pia “
1 comments:
Pesa ni kama maua,yanakuja na kuondoka hasa akili zikiwa sorry za viatu.
Post a Comment