24Bongo News :
Home » , » WANAFUNZI 5,157 WAFUKUZWA SHULE BAADA YA KUPATA UJAUZITO

WANAFUNZI 5,157 WAFUKUZWA SHULE BAADA YA KUPATA UJAUZITO

Wanafunzi 5,157 wa sekondari wamefukuzwa shule mwaka 2011 kutokana na kugundulika kupata ujauzito.

 

 Hayo yalielezwa jana jijini Dar es Salaam na mratibu wa mafunzo ya jinsia kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Winifrida Rutaindurwa katika semina ya waandishi wa habari kuhusu changamoto zinazowakabili watoto wa kike.

 Akizungumza katika semina hiyo iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), alisema idadi hiyo ambayo ni sawa na asilimia 6.8 ni ndogo ikilinganishwa na ya waliobainika kupata ujauzito na kufukuzwa mwaka 2010 ambao walikuwa 5,346 sawa na asilimia 8.1.

Kwa mujibu wa mtaribu huyo, katika utafiti wao wamebaini kwamba vyanzo vikuu vya tatizo hilo ni ukosefu wa usafiri wa uhakika kwa wanafunzi hao hali inayowafanya wengi wao hasa wanaosoma mijini kushawishika na lifti.

Vyanzo vingine ni umbali wa shule na maeneo wanayoishi, ukosefu wa mabweni kwa wanaosoma shule za kutwa na nyingine, matumizi mabaya ya teknolojia ikiwemo televisheni, mitandao ya kijamii kama face book, twiter na vingine.

Alisema ili kuepuka matatizo hayo, ni vyema jamii ikatambua kwamba watoto wa kike pia wanapaswa kupewa fursa kama walivyo watoto wa kiume hasa katika masomo.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard