Young Africans ambayo imeweka kambi ya mafunzo jijini Antalya itatumia mchezo huo kama fursa ya kujipima nguvu na timu hiyo la Denizlispor FC ambayo imeshuka kutoka ligi kuu ya Uturuki mwaka jana na hivi sasa inapamabana kurudi tena katika Ligi Kuu ya Uturuki.
Kocha Mkuu wa Young Africans Ernest Brandts amesema kwao ni furaha kupata nafasi ya kucheza na timu kubwa kama ya Denizlispor FC ambayo ina wachezaji wa kiwango cha kimataifa hivyo anaamini utakua ni mchezo safi na kuwavutia.
Young Africans imeendelea na mazoezi katika viwanja wa Fame Residecne tayari kabisa kujiandaa na mchezo huo utakaochezwa kesho katika uwanja wa Selen Football - Kalimya complex pembeni kidogo mwa mji wa Antalya.
Athumani Idd 'Chuji' na Hamis Kiiza waliokuwa wakijisikia vibaya kabla ya mchezo wa juzi dhidi ya Amrnini Bielefeld wanaendelea vizuri kabisa huku wakiendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wengine waliopo na timu mjini Antalya.
0 comments:
Post a Comment