24Bongo News :
Home » , » WANAFUNZI IFM WAANDAMANA BAADA YA WENZAO KULAWITIWA

WANAFUNZI IFM WAANDAMANA BAADA YA WENZAO KULAWITIWA

Wanafunzi wakiwa Wizarani.


Askari wakilinda usalama


Kamanda wa polisi kanda Maalum Suleiman Kova akimsikiliza mwanafuzi.




Wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha cha jijini Dar es Salaam (IFM) wameandamana leo majira ya adhuhuri hadi kwenye Wizara ya Mambo ya Ndani wakiwa na madai ya kunyimwa ulinzi na jeshi la polisi kwenye makazi yao ya hosteli za Kigamboni kutokana na kuvamiwa na majambazi mara kwa mara.

Wanafunzi hao walidai kuwa, siku ya Ijumaa walifanya kikao na jeshi hilo ili wawape ulinzi lakini suala la ajabu ni kuwa, siku waliyofanya kikao na Jeshi hilo ndiyo siku wenzao wawili wakiume walipovamiwa na kulawitiwa.

Majambazi hao wamekua wakidai wapewe laptops, simu na fedha na endapo kama mwanafunzi anakataa,basi umwingilia kinyume na maumbile.

Rais wa Serikali ya wanafunzi ya Chuo cha IFM alizungumza leo na Kamanda wa Polisi wa Kanda maalumu ya Kipolisi ya jiji la Dar es Salaam Suleiman Kova mara baada ya kuwasili eneo la ofisi za Wizara ya Mambo ya ndani ambapo alisema,
"Wanafunzi wenzetu wa kiume wamelawitiwa nyinyi tumewapa taarifa siku ya ijumaa kuwa hatuna ulinzi tunaibiwa hovyo vitu vyetu halafu siku hiyo hiyo unafanyika ubakaji huo…" 

Ndipo kamanda Kova aliwaamuru wanafunzi hao wafuatane naye waende hadi Kigamboni kwenye Kituo waliporipoti taarifa zao pamoja na kwenda kwenye Hosteli zao. Kova aliahidi kushughulikia jambo hilo kwa haraka bila kusita.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard