![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjenaefCDuZiOs2K31EXc16FuUevBv3tdMp8k4Lho9cKTLSA1OFuKefS5Iza0T9LjqxLARHCpd7QSCO5KrJdOsyeTsQT6gckYbhTytTtmhBGIBqn02cNLm_6qAZaygd7wb8Lx3VjUHRhHo/s640/kanga+moko7.jpg)
Kundi maarufu hapa jijini limeendelea kutia fora na kuwa gumzo kwa aina ya uchezaji wao.Serikali imekuwa ikifumbia macho suala hili kwani limekwepo kwa muda likiendelea kumomonyoa maadili ya kitanzania huku likichochea matendo ya ngono kwa vijana na jamii kwa ujumla.
Ni muda muafaka serikali ikaliangalia hili kwa jicho makini kwani hakuna tofauti na biashara ya kujiuza kwani matendo yao na uvaaji ni taswira tosha ya kutoendana na tamaduni ya kitanzania hasa ukizingatia wakati huu ambao taifa lipo kwenye changamoto ya kupunguza kama si kuondoa kabisa maambukizi ya Ukimwi.
Hivyo serikali ifanye mkakati wa kuzuia huu utamaduni mpya ambao ni sumu kwa taifa letu na kizazi hiki.