24Bongo News :
Home » » YANGA YAENDELEZA USHINDI LIGI KUU

YANGA YAENDELEZA USHINDI LIGI KUU

Young Africans leo imeendeleza wimbi lake la ushindi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom baada ya kuichapa tmu ya Tanzania Prisosns kutoka mjini Mbeya jumla ya mabao 3-1, katika mchezo uliofanyika jioni hii katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Young Africans ambayo inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 32 na mabao 28 ya kufunga, iliingia uwanjani kwa ajili ya kusaka pointi 3 muhimu ambazo imefanikiwa kuzipata.

Kikosi cha mholanzi Ernest Brandts kiliuanza mchezo kwa kasi, na kupata bao la kwanza dakika ya 11 kupitia kwa Jerson Tegete aliyemalizia pasi safi ya kiungo mshambuliaji Saimon Msuva.

Dakika sita baadae dakika ya 17, mshambuliaji wa Elias Maguli aliipatia Prisons bao la kusawazisha kufuatia uzembe wa walinzi wa Yanga kuzembea kumkaba mfungaji aliyekokota mpira toka upande wa pembeni mpaka alipofunga bao hilo.

Didier Kavumbagu alikosa mabao ya wazi dakika ya 7 na dakika 27 huku kiungo Nurdin Bakari akikosa pia bao la wazi dakika ya 38 ya mchezo.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza Young Africans 1-1 Prisons FC.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Yanga kuutawala mchezo hali iliyopelekea kujipatia bao la pili kupitia kwa mlinzi wa kulia Mbuyu Twite aliyemalizia mpira uliokolewa na walinzi wa Prisons kufuatia piga nikupige ya Nadir Haroub, na Saimon Msuvalangoni mwa lango la Prisons kabla ya mpira huo kumkuta Twite aliyeukwamisha wavuni.

Jerson Tegete aliendelea kuwa mwiba kwa timu ya Prisons baada ya kuipatia Young Africans bao la tatu dakika ya 66, akimalizia pasi safi ya kiungo Nurdin Bakari aliyetanguliziwa mpira na Hamis Kiiza na Nurdin kuwatoka walinzi wa Prisons kabla ya kumpasia Tegete aliyeukwamisha mpira wavuni bila ya ajizi.

Kama washambuliaji wa Young Africans wangekuwa makini Yanga ingeweza kuibuka na ushindi wa mabao mengi kwani Jerson Tegete alikosa bao la wazi baada ya kuwapinga chenga walinzi wote wa Prisons lakini umaliziaji wake haukuwa mzuri.

Mpaka mwisho wa mchezo Young Africans 3- 1 Prisons FC

Kiungo Frank Domayo aliugua ghafla na kuondolewa katika orodha ya wachezaji ya waliokuwa katika listi ya kuanza na nafasi yake ilichukuliwa na Nurdin Bakari, Domayo alijisikia kizunguzungu hali iliyompelekea daktari wa timu ya Yanga Dr Nassoro Matuzya kufukiria huenda akawa na malaria, baadaye Domayo alijisikia nafuu na kuutazama mchezo wote kwa dakika 90.

Kocha mkuu wa Yanga Ernest Brndts amesema anashukuru timu yake kupata kwa ushindi katika mchezo wa leo, kipindi cha kwanza wachezaji wangu hawakuwa makini na hawakuzingatia maaelekezo yangu , lakini wakati wa mapumziko niliwaeleza nini wanapaswa kukifanya na hatimaye timu ilibadilika na kuweza kutengeneza nafasi za kufunga mabao mawili japokuwa walikosa nafasi zingine za wazi

Kambi yetu ya mafunzo nchini Uturuki imetusaidia sana, wachezaji wanacheza kwa kujiamin ila kuna mapungufu madogo madogo yalijitokeza katika mchezo wa leo, benchi la ufundi tumeyaona na tutayafanyia kazi katika michezo itakayofuata alisema "Brandts"

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Mbuyu Twite/Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4.Nadir Haroub'Cannavaro', 5.Kelvin Yondani, 6.Athuman Idd 'Chuji', 7.Saimon Msuva, 8.Nurdin Bakari/David Luhende, 9.Didier Kavumbagu/Hamis Kiiza, 10.Jerson Tegete, 11.Haruna Niyonzima

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard