Hatimaye
mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba amepatanishwa na mama mzazi wa
Lulu baada ya mlolongo mrefu na mgumu wa jitihada za kuwapatanisha kina
mama hao wawili.
Chanzo cha habari cha kuaminika kimeripoti kwamba mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba alikua mzito kupatanishwa kwa sababu ya kukasirishwa na kitendo cha mama mzazi wa Lulu ambae hakuwahi kufika msibani wala kutuma salamu za pole kwa mama Kanumba.

Baada ya
Lulu kutoka kwa dhamana, mama mzazi wa marehemu Kanumba alisema yuko
tayari kuonana na Lulu kwa sababu ni mtoto na hana tatizo nae lakini
akasisitiza kama Lulu atakwenda kuonana nae ni sawa ila asiende na mama
yake.
Wazazi hao wamepatanishwa jumapili february 10 2013 ambapo Lulu alikuepo kama muhusika mkuu wakati huo wa upatanisho, kwa siku zote mwigizaji huyu alikua akiomba kupatanishwa na mama wa Marehemu, pia alikua akisisitiza kuomba mama yake apatane na mama Kanumba,

Sababu
za Mama Lulu kushindwa kwenda msibani alisema kwanza ni uoga kutokana
pia na jinsi vyombo vya habari vilivyopamba, na nyingine ni machungu
aliyokua nayo dhidi ya waigizaji hao wote wawili ambao alikua hajui
kama walikua wapenzi, alikua anajua Marehemu anamfundisha Lulu usanii
tu.
Mapatano yalisimamiwa na wazee wawili pamoja na watu wengine
wa karibu wa familia na ilichukua dakika 240 kazi kumalizika kutokana
na Mama mzazi wa Kanumba kuwa mgumu kiasi chake.
Baada ya kupatanishwa imeelezwa ndio mama mzazi wa Marehemu Kanumba, mama mzazi wa Lulu na watu wengine kadhaa wa karibu wa hizo familia, walikwenda kwenye kaburi la marehemu Steven Kanumba Kinondoni Dar es salaam.

0 comments:
Post a Comment