Home »
Elimu
,
Kitaifa
,
Matukio
» HAYA NDO MAJIBU YA BAADHI YA VIJANA TAIFA LA LEO NA KESHO KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
HAYA NDO MAJIBU YA BAADHI YA VIJANA TAIFA LA LEO NA KESHO KATIKA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE
WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
inaweza kukumbwa na kashfa kubwa kutokana na matokeo mabaya ya kidato
cha nne ya 2012 yaliyotangazwa juzi na Waziri wake, Dk Shukuru Kawambwa.
 |
| Katibu
Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako
akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa
kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. |
Kashfa hiyo inatokana na aina ya majibu yaliyoandikwa na baadhi
ya watahiniwa katika mitihani hiyo, huku wengine wakikusanya vitabu vya
majibu bila kujibu chochote, hali inayohusishwa na uhaba mkubwa wa
walimu katika baadhi ya shule za sekondari nchini.
Katibu Mtendaji wa
Baraza la Mitihani (Necta), Dk Joyce Ndalichako alisema wasahihishaji
walikutana na mambo ya ajabu yakiwamo matusi, michoro ya vitu
visivyoeleweka, mashairi na nyimbo za muziki wa kizazi kipya (bongo
fleva).
“Mwaka jana tulikutana na ‘single’ yaani waliandika mashairi
kwa uchache, lakini mwaka huu tumepata albamu nzima… ni vituko vitupu,
wengine wanaandika mapenzi, mwanafunzi anatumia ukurasa mzima
kumlalamikia mpenzi wake. Miongoni mwa yaliyoandikwa ni mpenzi,
umeniacha, natamani kunywa sumu, usiku silali nakuwaza wewe…” alisema Dk
Ndalichako.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili ofisini
kwake Dar es Salaam jana, Dk Ndalichako alisema wanafunzi wengine
waliandika malalamiko dhidi ya wabunge na uendeshaji wa Bunge.
“Unakuta mwanafunzi anaeleza anavyolishangaa Bunge… mtu
anaandika… nawashangaa wabunge, wamekaa kama wapo kijiweni, wabunge
wamekosa ustaarabu, badala kujadili kero za wananchi waliowachagua,
wanapokea timu zilizoshinda makombe… timu ikishinda Kombe la Kagame
inapokelewa bungeni. Bunge limekuwa kama kijiwe, bungeni siyo ukumbi wa
starehe kama mnataka kupokea timu hizo nendeni katika ofisi zao au
viwanjani…” alisema.
Alisema wanafunzi walioandika vitu visivyoeleweka walikuwa ni wengi na walichangia kwa kiasi kikubwa matokeo kuwa mabaya. Dk Ndalichako alionyesha baadhi ya michoro hiyo ambayo
inaonyesha vikaragosi ambavyo wanafunzi hao waliviita Messi (Lionel,
mchezaji wa Barcelona) na zombi (ni picha za kutisha) ambazo huonyeshwa
kwenye televisheni.
0 comments:
Post a Comment