24Bongo News :
Home » , » BAADA YA MAISHA KUBADILIKA UPEPO LULU SASA KURUDI SHULE

BAADA YA MAISHA KUBADILIKA UPEPO LULU SASA KURUDI SHULE

   BAADA ya kupata dhamana msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu ajipanga kujiendeleza na masomo ili aweza kupambana na changamoto za maisha.

Akizungumza na Maisha msanii wa filamu ambaye pia amekuwa ni mtu wa karibu wa  familia  ya Lulu Mahfudh Hussein 'Dkt. Cheni' amebainisha kuwa Lulu yupo kwenye mchakato wa kurudi shule ili aweze kuendelea na masomo yake

Alisema kuwa ingawa familia ina mikakati hiyo suala kubwa linalokwamisha kwa sasa ni kipato kwani familia yake haina uwezo wa kumlipia msanii huyo na badala yake anatakiwa Lulu kuanza kufanya kazi ili aweze kujikwamua kwa hilo

Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa kutokana na kipato cha familia ya msanii huyo hivyo anatakiwa kwa sasa aweze kufanya kazi ya filamu ili aweze kujimudu kama ilivyokuwa mwanzo na maisha yaendelee.

"Hapo awali alikuwa na uwezo wa kuihudumia familia yake kwa njia ya kazi zake alikuwa anamsomesha mdogo wake wa mwisho pamoja na kulipa kodi ya nyumba alikuwa akifanya mammbo mengi hivyo na swala la kusoma lijukumu lake pia" alisema

Mbali na hayo msanii Cheni alieleza kuwa Lulu yupo tayari kurudi shule ili aweze kujikwamua kielimu aweze kupambana na maisha hivyo jambo la msingi ni yeye kufikisha malengo yake aliyojipangia kwani umri wake bado ni mdogo na ana nafasi kubwa ya kubadilisha maisha yake

Akizungumzia kwa upande wa kazi Dkt. Cheni aliweka wazi kuwa endapo Lulu akimuomba amsimamie kazi zake atafanya hivyo kwani yote ni katika nia njema ya kumfikisha msanii huyo katika malengo aliyojipangia

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard