MTOTO wa kigogo Bongo aliyepata kuwa mbunge wa jimbo moja jijini Dar
es Salaam (jina kapuni) aliyetajwa kwa jina moja la Happy, amenaswa
gesti akiwa na Muddy aliyedaiwa kuwa ni mume wa mtu.....
Ukurasa
wa tipu unabainisha kuwa binti huyo alifanya kitendo hicho
cha aibu hivi karibuni maeneo ya Sinza kwenye nyumba moja ya kulala
wageni ambayo inasitiriwa jina lake kwa sasa.
“Alianza kutembea na
mume huyo wa mtu kwa muda mrefu, kosa alilofanya ni kupiga picha chafu
kwa kutumia simu yake,” chanzo kilianika mkasa.
Inaelezwa kuwa picha hizo zimesambazwa na rafiki mmoja wa msichana huyo kwa kinachodaiwa kutaka kuwaumbua wawili hao.