WENGI tunaamini kwamba ukishakuwa rais basi umeuvaa utajiri lakini kwake ni tofauti.Jose Alberto Mujica (77), Rais wa sasa wa Uruguay ambaye amevunja rekodi ya kuwa rais maskini zaidi kuwahi kutokea. Aliingia madarakani kwa tiketi ya chama cha Broad Front Machi Mosi, 2010.
Tofauti na marais wote duniani, Mujica haishi ikulu badala yake anaendesha maisha yake eneo la mashambani, mbali kabisa na mjini anakojishughulisha na ukulima wa maua na mazao mengine. Kabla ya kuwa rais, Mujica aliwahi kuwa waziri wa mifugo, wanyama na uvuvi tangu 2005 hadi 2008 alipochaguliwa kuwa seneta na baadaye kuwa rais.
Kwa nini ni Maskini?
Haamini uwepo wa mungu(atheist),huchangia asilimia 90 ya mshahara wake kwa watu fukara,yatima na wafanyabiashara wadogo wadogo wa kima cha chini huku kiasi kinachobaki anakitumia kununua chakula na pembejeo kwa ajili ya kilimo.
Usafiri wake
Mujica anamiliki gari dogo na chakavu maarufu hapo zamani kama Mgongo wa chura,na anamiliki gari moja tu ambalo analitumia katika shughuli za mizunguko yake kwa sababu alitumii mafuta sana na gharama za matengenezo ni kidogo kwani halisumbui mara kwa mara.
Alipotokea
Mujica amezaliwa katika familia ya wahamiaji kutokea Italy ambayo ilijihusisha na ukulima wa zabibu na maua,hivyo Mujica alikulia na kulelewa mashambani mpaka pale alipoanza kujiusisha na siasa kwenye chama cha wapiganaji wa msituni(guerila).Huyu ndie Jose Mujica rais maskini kuliko wote ambae hali nyama na hakuwahi kuishi Ikulu badala yake alikaa huko mashambani nje ya mji akilima maua.Awali kabla hajawa rasi alikuwa waziri wa Mifugo,wanyama na Uvuvi tangu 2005 hadi 2008 kabla ya kuteuliwa kuwa seneta na baadae Rais.
HONGERA JOSE MUJICA
VIONGOZI WA AFRIKA WAJIFUNZE KITU HAPO KULIKO KUJILIMBIKIZIA UTAJIRI.