Kwa zaidi ya wiki tatu zilizopita, kuanzia tarehe 19 Januari 2013 
mpaka 10 Februari 2013 mashabiki wa soka barani Afrika na duniani kote 
walikuwa hawabanduki katika viti vyao au sofa kwa ajili ya kutizama 
mashindano makubwa kabisa ya soka barani Afrika ya kuwania Kombe la 
Mataifa Ya Afrika mashindano ambayo kwa kizungu yanajulikana kama Orange
 Africa Cup Of Nations.
Wenyeji wa mashindano ya mwaka huu walikuwa Afrika Kusini. Jumla ya 
mechi 32 zilichezwa na zote zilionyeshwa Live bila chenga kupitia 
channels za SuperSport zinazopatikana kupitia DStv, wakongwe wa 
digitali.
Wakati wa fainali, DStv kupitia kampuni mama ya MultiChoice Tanzania 
walijumuika na mashabiki wa soka na wadau mbalimbali visiwani Zanzibar 
katika viota vya Gymkhana Club na Mtoni Marine. Huko palikuwa na special
 screening ya mchezo huo wa fainali ambapo Nigeria waliibuka mabingwa 
(kwa mara ya tatu sasa) baada ya kuwalaza Burkina Faso kwa goli 1-0.
Kwa mapana na marefu umekuwa msimu wa kufurahi na marafiki na pia 
kutizama jinsi ambavyo kabumbu linazidi kutamba kama mchezo unaopendwa 
zaidi sio tu Afrika bali duniani kote.
 


 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment