Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji watatu, Johnston Busingye,
Marystella Amoko na Jean Bosco Butasi katika mahakama hiyo jijini Arusha
ambapo upande wa serikali uliwakilishwa na wakili Mark Mwalambo na
upande wa mlalamikaji unawakilishwa na wakili Edson Mbogoro.
Katika kesi hiyo ya marejeo namba 7 ya mwaka 2012 iliyofunguliwa katika mahakama hiyo, Komu ambaye alikuwa mgombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, anapinga utaratibu uliotumika kupata wagombea wa ubunge kutoka Tanzania kwani ulikiuka ibara ya 50 ya Katiba ya Afrika Mashariki inayosema kuwa wabunge watapatikana kwa uwiano.
Awali Januari 31 mwaka huu katika mahakama hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alilalamikiwa mahakamani hapo kwa kushindwa kujibu hoja ndani ya siku 45 alizopewa.
Katika utetezi wake, Mwanasheria Mkuu alitoa sababu nne za kwa nini hakujibu ndani ya muda aliopangiwa, akisema kuwa kulikuwa na kesi kama hiyo ikisikilizwa mjini Dodoma, na kwamba alitoa sababu kuwa walikuwa hawajajua viwango vya ada za kesi hiyo.
Aliongeza kuwa walikuwa wanatafuta wanasheria wa mahakama ya Afrika Mashariki ili waweze kupata tafsiri za kisheria kwa mambo yaliyowasilishwa.
Katika sababu ya mwisho alidai kwamba kwa kuwa suala hilo lina maslahi ya nchi na jumuia yenyewe, ilibidi liangaliwe kwa umakini ili Tanzania isikose haki.
Madai hayo yote yametupiliwa mbali na jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo, hivyo kumuamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujibu hoja zilizotolewa mahakamani hapo ndani ya siku 15 na kulipa gharama za mlalamikaji.

source:freemedia
Gustav Chahe, Iringa
0 comments:
Post a Comment