24Bongo News :
Home » , » MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUJIBU HOJA YA MBUNGE WA CHADEMA EAC NDANI YA SIKU 15

MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KUJIBU HOJA YA MBUNGE WA CHADEMA EAC NDANI YA SIKU 15

Jopo la Majaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki, limemwamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania kujibu hoja zilizowasilishwa mahakamani hapo na Anthony Komu (CHADEMA) ndani ya siku 15 na kumlipa mlalamikaji huyo gharama katika hatua za pingamizi za awali.
 
Kesi hiyo inasikilizwa na jopo la majaji watatu, Johnston Busingye, Marystella Amoko na Jean Bosco Butasi katika mahakama hiyo jijini Arusha ambapo upande wa serikali uliwakilishwa na wakili Mark Mwalambo na upande wa mlalamikaji unawakilishwa na wakili Edson Mbogoro.

Katika kesi hiyo ya marejeo namba 7 ya mwaka 2012 iliyofunguliwa katika mahakama hiyo, Komu ambaye alikuwa mgombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki, anapinga utaratibu uliotumika kupata wagombea wa ubunge kutoka Tanzania kwani ulikiuka ibara ya 50 ya Katiba ya Afrika Mashariki inayosema kuwa wabunge watapatikana kwa uwiano.

Awali Januari 31 mwaka huu katika mahakama hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, alilalamikiwa mahakamani hapo kwa kushindwa kujibu hoja ndani ya siku 45 alizopewa.

Katika utetezi wake, Mwanasheria Mkuu alitoa sababu nne za kwa nini hakujibu ndani ya muda aliopangiwa, akisema kuwa kulikuwa na kesi kama hiyo ikisikilizwa mjini Dodoma, na kwamba alitoa sababu kuwa walikuwa hawajajua viwango vya ada za kesi hiyo.

Aliongeza kuwa walikuwa wanatafuta wanasheria wa mahakama ya Afrika Mashariki ili waweze kupata tafsiri za kisheria kwa mambo yaliyowasilishwa.

Katika sababu ya mwisho alidai kwamba kwa kuwa suala hilo lina maslahi ya nchi na jumuia yenyewe, ilibidi liangaliwe kwa umakini ili Tanzania isikose haki.

Madai hayo yote yametupiliwa mbali na jopo la majaji wanaosikiliza kesi hiyo, hivyo kumuamuru Mwanasheria Mkuu wa Serikali kujibu hoja zilizotolewa mahakamani hapo ndani ya siku 15 na kulipa gharama za mlalamikaji.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard