Wakati zikiwa zimebaki wiki chache
tu hadi kifo cha Stephen Kanumba kitimize mwaka mmoja, aliyekuwa mpenzi
wake, Elizabeth Michael aka Lulu kwa mara ya kwanza leo ameandika ujumbe
kuhusiana na jinsi anavyomkumbuka.
Lulu aliachiwa kwa dhamana mwezi January mwaka huu baada ya kukaa
mahabusu kwa takriban miezi minane kufuatia kukamatwa kwa kuhusika na
kifo cha Kanumba.
Lulu ambaye hivi karibuni amekuwa akitweet mara kwa mara ameandika:
“
Ulikuwa zaidi ya
baba,kaka,mpenzi,mume,ndugu,rafiki….sitoacha kukulilia katika maisha
yangu yote!!R.I.P daddy angu STEVEN KANUMBA.”
Akiambatanisha na picha ya Kanumba, Lulu ameongeza, “I will alwayz love u daddy angu
!”