NANCY AZINDUA KITABU CHA MTOTO NYOTA YAKO
MATUKIO KATIKA PICHA
Akizungumzia kasumba ya watanzania wengi kutopenda kusoma vitabu na
jinsi alivyokabiliana nayo Nancy anasema, “nilimshirikisha mchoraji
mzuri sana kwasababu nilitaka kumvutia mtu kwa wepesi kwanza kiwe
kifupi, yaani kidogo. Ni kitabu ambacho unaweza kukipitia ndani ya
dakika tano. Kuna picha nyingi lakini meseji yake ni nzito sana.”
Kwa upande wake Profesa Mwaikambo(74), ambaye mwaka huu ubalozi wa
Marekani ulimtunuku tuzo ya haki ya Dk Martin Luther King amempongeza
Nancy kwa kuandika kitabu hicho na kusema kuwa watoto wengi hasa wenye
kuanzia umri wa miaka mitatu wataweza kukifurahiia kwa kuangalia picha
tu.