24Bongo News :
Home » » AZAM YATETEA KOMBE MAMPINDUZI CUP

AZAM YATETEA KOMBE MAMPINDUZI CUP



Washindi wa pili wa ligi kuu Tanzania bara 201!1/12 Azam fc wamekuwa wa kwanza kutetea ubingwa wa Mapinduzi kwa timu toka Tanzania Bara huku ikiwa ya pili kwa historia kwa vilabu vyote ambapo Miembeni ndio wa kwanza kutetea ubingwa huo wa Mapinduzi.

Nahodha wazamani wa timu za vijana za taifa na Azam academy Himid Mao jana aliiongoza Azam fc kuifunga Tusker ya Kenya goli 2-1 katika mchezo wa fainali ya kombe la mapinduzi uliochezwa katika uwanja wa Amani na kumpatia fursa Himid ya kunyanyua kombe kana nahodha toka afanye hivyo katika masgindano ya Uhai cup mara mbili mfululizo.

Katika mchezo huo azam walikuwa wa mwanzo kufika katika lango la wapinzani wao na kushindwa kuingiza mpira wavuni, huku kiungo wa Azam fc toka Ivory coast Micgael Bolou akitawala eneo la kati katika kipindi cha kwanza huku azam na tusker wakishambuliana kwa zamu.

Alikuwa Jesse Were aliyeipa goli la kuongoza Tusker katika dakika ya 60 likiwa goli lake la 5 na hivyo kumuwezesha kuwa mfungaji bora wa michuano hii ya mapinduzi cup.

Katika dakika ya 66 azam walifanya mabadiliko ya kumtoa Uhusu Selemani na kumuingia chipukizi aliyesajiliwa na azam fc akitokea Ruvu shooting katika dirisha dogo la usajili Abdallah Seif.

Kuingia kwa Abdallah Seif kuliongeza kasi ya ushambuliaji ya azam na dakika ya 70 Joseph Chikokoti alishika mpira uliopigwa na Abdallah Seif kwenda kwa Khamisi Mcha na kuzaa penati iliyoipatia goli la kusawazisha kwa azam kupitia kwa Joackins Atudo akifunga goli lake la 4 katika michuano hiyo.

Azam na tusker waliendelea kushambuliana kwa zamu na kupoteza nafasi za kujipatia magoli ya ushindi na kupelekea dakika 90 zikiisha wakiwa sare ya goli 1-1 na kupelekea kuongezwa dakika 30

Azam fc walipata goli la ushindi ndani ya dakika 30 za nyongeza ikiwa ni dakika ya 93 kupitia kwa Gaudency Mwaikimba akiunga mpira wa Himid Mao na kupelekea mchezo kumalizika kwa Azam kuibuka na ushindi wa goli 2-1 na kutwa ubingwa huo.

Katika mchezo huo wa fainali hapo jana katika dkika ya 90 mmama anaedaiwa ana matatizo0ya kiakili alikatisha uwanjani akiwa ameshija karatasi yenye maandishi.

Jesse Were kutoka tusker ndixe aliyeibuka mfungaji bora katika mashindano hayo yanayokwenda sambamba na sherehe za mapinduzi Zanzibar.



TIMU ZILIZOWAHI KUTWAA UBINGWA WA MAPINDUZI

Miembeni 2008 na 2009
Mtibwa sugar 2010
Simba sc 2011
Azam fc 2012 na 2013

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard