24Bongo News :
Home » , » MTWARA HALI YAWA TETE,NYUMBA ZACHOMWA NA VURUGU KIBAO

MTWARA HALI YAWA TETE,NYUMBA ZACHOMWA NA VURUGU KIBAO

Taarifa za redio mbao ambazo hazijathibitishwa na Mamlaka yeyote hadi hivi sasa ni kwamba wananchi wanaendelea kufanya uharibifu mkubwa huko ambapo naambiwa wamevamia gereza wakafungulia wafungwa na kisha kupiga moto gereza.
 

Polisi wamezidiwa na wamejifungia kituoni wanarusha mabomu yao tokea huko walikojificha maana nje hakutamaniki. Na wameshateketeza nyumba ya mama Anna Abdallah.





Taarifa hizi ni kwa mujibu wa Blog ya MTWARA KUMEKUCHA …...

Updates

Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama kinaendelea kwa kuwashirikisha maafisa wa polisi na maafisa usalama waliotoka Dar es Salaam kuongezea nguvu.
Maaskari na makachero wamewasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.Maaskari na makachero wawasili Mtwara leo asubuhi na helkopta kuongezea nguvu.
Hosteli ya wanafunzi wa chuo cha Utumishi maeneo ya Kiyangu B Mtwara yakoswa koswa kuchomwa moto kwa kile kinachodhaniwa kuwa na uhusiano na Hawa Ghasia mpaka sasa wanafunzi hawana mahala pa kukaa.
Kituo kidogo cha Polisi Cha Shangani mkoani Mtwara nacho chakoswa na moto. Ofisi ya Afisa Mtendaji Nkanaledi mkoani Mtwara nayo yavunjwa.
Wananchi wamechoma moto mahakama ya Mwanzo na kuvunja vioo vya nyumba za waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.
Wakiwa katika mahakama ya mwanzo, Polisi walizingirwa na vijana waliokuwa wamebeba mawe na kufunga barabara zote za kuingia na kutoka Kituo Kikuu cha Mabasi na eneo la Soko Kuu, licha ya kufyatua hewani mabomu ya machozi.
Baadhi ya barabara za zimezibwa kwa kuchomwa matairi ya gari, na kuongeza hofu kwa wananchi.
Hali imeshakuwa mbaya Masasi taarifa zilizotufikia punde wamechoma eneo linaloitwa loliondo, ofisi za elimu na ofisi ya trafiki, inasemekana jamaa wameshavamia ofisi za halmashauri wengine wako njiani nyumbani kwa mama Ana Abdala, hapa Mtwara mjini maduka yote eneo la soko kuu na stendi yamefungwa hakuna huduma, huko Newala , leo kuna mkutano mkubwa mchana huu wa kumkataa George Mkuchika.
Vurugu zahamia wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Nyumba ya Mbunge wa Masasi nayo yateketezwa kwa Moto hivi sasa...Madereva Bodaboda waandamana ...Vurugu zashamiri 


Mabomu Kibao..Hali ni tete Askari auawa
Na taarifa zaidi kutoka Masasi zinaeleza kuwa askari wa upelelezi Masasi aliyejichanganya katika vurugu wananchi walimshitukia akiwapiga picha, akashambuliwa na kuuliwa. Askari huyo inaelezwa amekutwa na bastola mbili. Taarifa zaidi baada ya kuthibitishwa tutawaletea

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard