24Bongo News :
Home » , » WEMA NA MAMA YAKE WAMALIZA BIFU LAO

WEMA NA MAMA YAKE WAMALIZA BIFU LAO


Msanii maarufu kwa kazi zake nzuri na skendo kibao Wema Sepetu na mama yake, Mariam Sepetu wamemaliza bifu lao, sasa ukiwaona ni kama kumbikumbi......

Hivi karibuni kwenye Arobaini ya mama wa Mtangazaji wa Kipindi cha Take One, Zamaradi Mketema, nyumbani kwao Kinondoni-Studio, Dar, Wema alibambwa akimfuata mama yake aliyekuwa pembeni na kumkumbatia huku akimdekea.

Mama na mwana hao waliendelea kubembelezana na kuwafanya watu waliokuwa eneo hilo kuwashangaa kutokana na kumbukumbu za hivi karibuni ambapo walitofautiana kiasi cha Wema kukataa mama yake asifike kwake.

Akizungumza na mwandishi wetu baada ya kuwakuta wamekumbatiana, mama Wema alisema:

“Nampenda sana mziwanda wangu huyu, we’ acha tu, japokuwa muda mwingine ananikosea. Unajua napenda kuwa naye muda wote lakini kutokana na majukumu aliyonayo kuonana ni tabu, lakini Wema kwangu bado ataendelea kuwa mtoto siku zote.”

Aidha, wakiwa wanaendelea kupiga stori za hapa na pale, mama huyo alimchombeza bintiye kuhusu kula ice cream
ambapo Wema alidakia na kumwambia mama yake kuwa asijali wakimaliza shughuli za arobaini hiyo watakwenda.

“Usijali mama yangu, tukimaliza hapa tutakwenda. Mimi nipo wala huwezi kukosa kitu ambacho unakitaka,” alisema Wema.

Mwishoni mwa mwaka jana, Wema alimkasirikia mama yake huyo kufuatia kuanika runingani mambo ambayo binti yake hakuyapenda yawe wazi.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard