Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya vodacom simba sc wamebanwa tena na timu ya jeshi la kujenga taifa (JKT) na safari hii walikuwa ni wakutokea Oljoro jijini Arusha.Simba sc walikuwa katika uwanja wa shekh Amri Abeid jijini Arusha kuwakabili JKT Oljoro katika muendelezo wa ligi kuu ya vodacom.
Simba wakiwa wametoka kutoa sare ya na JKT Ruvu waliuwanza mchezo vyema kwa kutawala kipindi cha kwanza na katika dakika ya 6 Mwinyi Kazimoto aliachia shuti la umbali wa mita 30 na kutinga moja kwa moja nyavuni.Kipindi cha pili hakikuwa kizuri kwa simba kufuatia Oljoro kulisakama lango la simba na kama wangekuwa makini wangetoka na ushindi wa goli 3.
Alikuwa Paulo Nongwa katika dakika ya 54 ajipo isawazishia Oljoro na kupelekea mchezo kumalizika kwa sare ya goli 1-1.
0 comments:
Post a Comment