Hatimaye lile Sakata la Migogoro ya Ardhi ambayo imedumu kwa muda mrefu Wilayani Manyoni Kufuatia Shinikizo la Wananchi kuwaondoa Maafisa Ardhi limefanikiwa baada ya Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk.Perseko Vicent Kone Kuwasimamisha Kazi kwa muda usiojulikana Maafisa Ardhi watatu ambao ndio walikuwa wakilalamikiwa sana na wananchi ambapo Mkurugenzi wa Halmashauri Bi.Fotunata Marya kunusurika kutokana na uchache wa malalamiko dhidi yake ambapo wananchi wawili tu ndio waliweza kulalamikia utendaji kazi wake.
Katika Mkutano wa Hadhara uliofanyika katika viwanja vya Mnadani eneo la Majengo wilayani Manyoni ambapo Mkuu wa Mkoa wa Singida alikuwa katika ziara yake ya kikazi aliwaruhusu wananchi 45 kutoa kero mbalimbali ambazo zinawakabili.
Mtandao huu uliwahi kuandika ziara ya Mkuu wa Wilaya Manyoni Bi.Fatma Hassan Toufiq ambapo wananchi wa eneo la Majengo na Kipondoda walimuomba kumtimua Kazi Afisa Ardhi Leonard Msafiri kwakuwa amekuwa kero kubwa katika wilaya ambapo alikuwa akipora viwanja vya wananchi pasipo kufuata taratibu wala kuwalipa fidia wananchi wanaomiliki maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Singida katika ziara yake ya siku tatu wilayani Manyoni akiwa katika eneo la Majengo na kipondoda aliweza kukutana na madudu ambayo yalikuwa yakifanywa na Maafisa ardhi ambapo wananchi 45 waliweza kutoa kero zao kuhususiana na kuporwa meneneo yao bila kulipwa fidia na maafisa wa ardhi ambao walikuwa wakitajwa kwa majina huku baadhi ya watoa kero wakilia kwa uchungu na kumuomba mkuu wa mkoa kuingilia kati sakata hilo ambalo limedumu kwa miaka mingi bila ufumbuzi.
Akijibu kero zao katika mkutano wa Hadhara DK.Kone alisema amesikia kilio cha wananchi wa Manyoni na kuanzia sasa
“Ninasimamisha Shughuli zote za ugawaji na upimaji wa Viwanja wilayani Manyoni mpaka pale maeneo yote yanayolalamikiwa yawe yamepatiwa ufumbuzi,na nimesimamisha shughuli zote za ujenzi kwenye maeneo yote yanayolalamimikiwa,na Kuanzia sasa nawasimamisha Kazi Maafisa Ardhi wanaolalamikiwa Bw. Leonard Msafili,John Chima na Kenedi Chigulu ambao wamesababisha malalamiko haya”.
Kuhusu suala la Mkurugenzi naombeni mnipe muda.