Hospitali
ya Kairuki imeasema inajiandaa kujenga kituo cha kisasa kwa ajili ya
kutoa huduma kwa kina mama zikiwamo za wanawake wasiopata mimba na hivyo
kuwazalisha kwa kutumia chupa.
Hatua hiyo ni sehemu ya mipango
ya baadaye itakayotelekezwa na hospitali hiyo ambayo kesho itaadhimisha
miaka 25 tangu kuanzishwa kwake na muasisi wake, Marehemu Profesa Hubert
kairuki mwaka 1987.
Akizungumza
na wahariri wa vyombo vya habari kuhusiana na maadhimisho hayo,
Mkurugenzi Mkuu wa hospitali hiyo, Dk. Asser Mchomvu, alisema kuwa mbali
na ujenzi wa kituo hicho, hospitali yake itanunua mashine ya kisasa ya
uchunguzi T Scan, kufungua matawi ya hospitali hiyo mikoani, kusitisha
upasuaji wa kutumia visu, kutoa elimu kwa umma na kuendelea kushirikiana
na serikali katika sekta ya afya.
Dk. Mchomvu lisema kuwa
hospitali hiyo imetoa huduma mbalimbali za bure za kusaidia jamii kama
sehemu za madhimisho hayo kama utoaji wa tiba ya bure, dawa, madawati na
vifaa vya tiba iliyogharimu Sh. milioni 12.
Alisema kuwa licha
ya changamoto mbalimbali walizokutana nazo, hospitali hiyo imefanikiwa
kuanzisha chuo kikuu cha kwanza binafsi nchini.
Aidha,
imefanikiwa kubuni na kuanzisha mfumo wa kumkukumbu za wagonjwa
unaotumia mtandao wa kompyuta badala ya kutumia kuhifadhi kumbukumbu
hizo kwa kutumia mafaili.Kwa mujibu wa Dk. Mchome, hospitali ya
Kairuki imetoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 4,000 za moja kwa moja na
zisizo za moja kwa moja.
Kuhusu Chuo Kikuu cha Kairuki, Dk. Mchome alisema tangu mwaka 1998, limeshazalisha wahitimu 971.
Akizungumzia
ujenzi wa kituo cha wanawake, Naibu Mkurugenzi Mkuu, Dk. Clementina
Kairuki-Mfuka, alisema ujenzi huo wa jengo la ghorofa sita utaanza baada
ya kukamilikataratibu zote na kwamba utagharimu Sh. bilioni 7.2.
Dk.
Clementina ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake,
alisema jengo hilo litakuwa na kuduma mbalimbali kama maegesho ya
magari, sehemu ya dawa, maabara, vyumba vya kulaza wagonjwa na ofisi za
madaktari. Vile vile pembeni utajengwa uwanja mdogo wa helikopta.
CHANZO: NIPASHE
0 comments:
Post a Comment