- Mpira wa kufurahisha mashabiki bila malengo hauna manufaa...
- Taifa Stars hii haiwezi kushinda mechi ugenini kama washambuliaji hawatorekebisha makosa.
- Timu nyingi zinapokuja kucheza Ugenini zinakuwa na mbinu mbadala wa kuhakikisha zinatoka na matokeo mazuri...
Ni pongezi kwa Kocha na benchi la Ufundi kwa namna timu ilivyocheza hasa kwa kipindi kifupi timu ilivyoandaliwa .Hii ni positive kwa maendeleo ya soka na jinsi watanzania tunapotamani kufika na kufuta ule uteja wa miaka mingi kwenye michuano mikubwa.
![]() |
Kikosi cha Taifa Stars |
Kwa namna timu ilivyocheza na haina ya wachezaji tulionao ni jambo zuri kuona timu ikiweka mpira chini na kucheza bila papara.Kitu kimoja ambacho bado tunakikosa ni matumizi ya nafasi tunazozipata kwenye ushambuliaji na namna washambuliaji wetu wanapokosa umakini.
Mpira wa sasa ni mpira wa mbinu,malengo na kutumia makosa ya timu pinzani.Tutacheza mpira wa pasi na kuwafurahisha mashabiki lakini kama tutakosa mbinu za kimchezo na timu kutokuwa na malengo hasa pale inapokuwa imeidhibiti timu pinzani hatuna budi kujiiuliza upya na kurekebisha matatizo hayo.
Ni kazi ngumu kwa timu yetu kwenda ugenini nchini Nigeria na kurudi na ushindi kwa sababu hatuna mbinu sahihi kulingana na mechi tunazocheza.Mfano..tumekuwa tukishuhudia timu ya taifa na vilabu vinavyotuwakilisha kwenye mechi za kimataifa hasa tunaposhambuliwa ama kuzidiwa wachezaji wetu hukosa nidhamu ya mchezo wakati mwingine kushindwa kucheza kitimu na kimbinu.
Timu kubwa zenye uzoefu zinapokuwa ugenini hucheza kwa tahadhali kubwa na kwa malengo zaidi hasa zinapozidiwa kimchezo na kutumia udhaifu wetu kupata matokeo uwanjani.Nigeria hii tusitegemee itacheza hivyo nyumbani jijini Lagos.
Hivyo ni lazima kuhakikisha tunatumia mechi za nyumbani kupata ushindi kwa kucheza kitimu ,nidhamu na kimbinu .Mwanzo mzuri wa benchi la Ufundi chini ya kocha Mkwasa na sasa kurekebisha makosa na kumpa muda zaidi kuweza kuleta mabadiliko ya mchezo wa soka nchini kwa ngazi ya taifa na vilabu pia.
By JR.