- Diego Costa alioneka akimpiga kiatu kwenye mbavu beki wa Liverpol Martin Skrtel
- Wachezaji hao walikuwa wameanguka chini baada ya Costa kumchezea faulo beki huyo
- Wachezaji hao walishakwaruzana tena kipindi cha nyuma
- Hivi karibuni alifungiwa mechi tatu baada ya kukwaruzana na Beki wa Arsenal Gabriel
Mchezaji tegemeo wa Chelsea mshambuliaji Diego Costa huenda akafungiwa tena baada ya jana Refa kushindwa kuona tukio hilo ndani ya uwanja pale Costa alipofanya madhambi hayo huku wakiwa wanaanguka chini ndipo mchezaji huyo aliponyanyua mguu wake na kumpiga mbavuni mchezaji huyo.Skrtel akuonekana kushtushwa na tukio hilo japo lilikuwa wazi
Chama cha Soka cha Uingereza FA huenda kikamfungia endapo kitafanya replay ya tukio hilo na kupitia report ya mchezo huo.
Akizungumza na BT sport aliyewahi kuwa Refa wa ligi hiyo Howard Webb alisema...
"Ilikuwa na tukio la kadi nyekundu.FA itawabidi kulitazma upya.Nafikiri ni kadi nyekudu kwani alimfanyia faulo Martin Skrtel na pia kulikuwa na tukio la pili.Tukio la pili ni kosa na adhabu yake ni kadi nyekundu.Mark Clattenburg alikuwa karibu na tukio hilo na ni vigumu kusema hakuweza kuliona tukio hilo.
Aliendelea kusema.."FA uwa hawachukui hatua ikiwa refa alikuwa akitazama tukio hilo ila nadhani kuwa unatazama tukio haimaanishi uponafocus hapo.Diego alikuwa na bahati kuendelea kuwepo uwanjani hapo."
0 comments:
Post a Comment