Staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ yamemkuta ni sawa, kisa ni ile ishu yake ya kutengeneza filamu inayoitwa Sister Marry ambapo mapadri wamemtaka asiipeleke sokoni milele.
Katika kikao hicho kizito kilichotumia takribani saa 4 na dk 49 kilichofanyika Jumanne iliyopita katika Ofisi za Utamaduni jijini Dar es Salaam.
Washiriki wa kikao hicho walikuwa Ray, Mkurugenzi Mtendaji wa Utamaduni aliyetajwa kwa jina moja la Mwansoke, mapadri wanne na mtu mmoja aliyedaiwa kuwa ni wa kutoka Ofisi za Usalama wa Taifa.
0 comments:
Post a Comment