Barabara eneo la Dumila ikiwa imefungwa. |
Malori yakiwa yamepaki baada ya wananchi wenye hasira kufunga barabara. |
Mkuu wa mkoa wa Mororgoro,Joel Bendera akizungumza na wananchi hao. |
Polisi wakilinda usalama eneo la tukio. |
Kikao cha dharura cha kamati ya ulinzi na usalama. |
Afisa Tabibu wa Zahati ya Dumila Dr Mathew Kayunga |
Bwana Kayunga arithibitihsa kupokea majeruhi saba waliojeruhiwa kwenye vulugu hizo na kudai kwamba alipokea marehmu mmoja Bw Mohamed Msigala[60] mabye alidai kwamba bado hawajaufanyioa uchunguzi mwili wa marehemu huyo hivyo hawezi kuthibitisha ni kitu gani kimemuua.ingawa alikili kwamba marehemu huyo alifikishwa kwenye Zahanati hiyo kwa usafiri wa boda boda akiwa tayari ameshakufa huku mwili wake ukiwa na jeraha kidevu na sikio lake la kulia lilikuwa likivuja damu. Baba mdogo wa marehemu huyo Bw Salum Hussein Mnyika[69] alipohojiwa na mtandao huu alidai kwamba kwa kipindi kirefu mwanaye huyo alikuwa akisumb uliwa na ungonjwa wa moyo mkubwa.
"Mwanangu ni mkazi wa kijiji hicho cha Mwabwegele kinachogomanai wa na wafugani pamoja na wakulima hivyo leo asubuhi alijumuika na wenzake kwenye maandamo hayo ya kufunga barabara na kwamba alitoka kwenye kijiji hicho kwa kutumia usafiri wake wa baiskeli na kwamba aliichacha baiskeli yake nyumbani kwangu na kwenda kujiunga na wenzake saa sita najulishwa kwamba amefariki huenda mstuko ule wa mabomu umestua moyo wake"alisema Bw Mnyika.
0 comments:
Post a Comment