TIMU ya taifa ya Mali jana imeifunga mabao Ghana 3-1 na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika, wakiipiku Black Stars kwa mwaka wa pili mfululizo kwenye mashindano haya.
Mshambuliaji Mahamadou Samassa alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 21, Nahodha Seydou Keita akafunga la pili dakika ya 48 na Sigamary Diarra akahitimisha karamu hiyo ya mabao.
Kwadwo Asamoah aliifungia Ghana bao la kufutia machozi dakika ya 82. Mshambuliaji wa Ghana, Wakaso Mubarak alikosa penalti mapema kipindi cha pili.
Mwaka jana, Mali iliifunga Ghana 2-0 katika mechi ya kuwania nafasi ya tatu. Waliingia kwenye michuano ya mwaka huu wachezaji wakisema wamedhamiria kufanya vizuri ili kuwapa faraja mashabiki wao kwa vurugu za kisiasa zinazoendelea nyumbani kwao.
Kipigo cha jana ni pigo lingine kwa Ghana, baada ya kuingia Nusu Fainali kwa mara ya nne mfululizo bila kuingia Fainali.
Ghana iliingia kuwania nafasi ya tatu baada ya kutolewa na Burkina Faso kwa mikwaju ya penalti kwenye Nusu Fainali. Black Stars walitwaa taji la mwisho la Mataifa ya Afrika mwaka 1982.
Kikosi cha Mali:
Soumaila Diakite, Diawara, Salif Coulibaly, Adama Coulibaly, Tamboura, Ousmane Coulibaly, Kalilou Traore, Mahamane Traore, Mahamadou Samassa (Sigamary Diarra 78), Keita, Diabate.
Benchi: Mamadou Samassa, N'Diaye, Wague, Maiga, Sissoko, Idrissa Coulibaly, Cheick Diarra, Yatabare, Sow, Samba Diakite, Yirango.
Kadi ya njano: Tamboura.
Wafungaji wa mabao: Mahamadou Samassa 21, Keita 48, Sigamary Diarra 90.
Kikosi cha Ghana:
Dauda, Richard Boateng, Vorsah, Boye (Mensah 46), Afful, Wakaso,Awal, Asamoah, Asante, Atsu (Adomah 70), Gyan (Clottey 75).
Benchi: Agyei, Pantsil, Annan, Agyemang-Badu, Derek Boateng, Rabiu, Akaminko, Boakye, Kwarasey.Kadi za njano: Wakaso, Vorsah, Asante.Mfungaji wa bao: Asamoah dk82.
Mahudhurio: 6,000
Refa: Eric Otogo-Castane (Gabon)
0 comments:
Post a Comment