"SINA MPANGO WA KUOA STAR,MFANYAKAZI WA BENKI NDO NITAKAEMUOA" ASEMA RAY
Katika kile kilichotafsiriwa kuwa ni kuwafutilia mbali wasanii
wenzake, Blandina Chagula na Ruth Suka ‘Mainda’ aliowahi kudaiwa kutoka
nao kimapenzi, staa wa filamu Bongo, Vincent Kigosi amefunguka kuwa,
hatarajii kuoa msanii kwani anaogopa presha.
Akizungumza issue hii hivi karibuni, Ray alisema kuwa anajua matatizo
ya kuoa staa hivyo ili kuepukana nayo ameamua kuwekeza penzi lake kwa
mwanamke anayefanya kazi benki akidai kuwa
huyo ndiye tulizo la moyo wake.
“Kaa ukijua kuwa sina mpango wa kumuoa staa
yeyote, mwanamke ninayetarajia kumuoa ni mfanyakazi wa benki na mipango
yangu ikikamilika nitakueleza kila kitu. Mimi sitaki presha bwana,”
alisema Ray.