24Bongo News :
Home » » WIZARA YASHINDWA KUFAFANUA AJIRA DHIDI WAGENI

WIZARA YASHINDWA KUFAFANUA AJIRA DHIDI WAGENI



Wizara ya Kazi na Ajira, imeshindwa kutoa ufafanuzi kuhusu raia wa kigeni wanaoishi nchini na kufanya kazi za kawaida ambazo kisheria zinapaswa kufanywa na wazawa.

Katika mkutano kati ya wizara na waandishi wa habari jana, iliibuliwa hoja ya kwanini wageni wanaajiriwa kwenye baadhi ya mahoteli makubwa na makampuni kufanya kazi hizo za kawaida.

Licha ya kukiri kuwepo hali hiyo, Mkurugenzi Msaidizi wa wizara hiyo, Ally Msaki, alijitetea kuwa wageni hao wamekuwa wakiwapatia vibali hivyo kutokana na elimu zao.

Hata hivyo, utetezi huo unakuja wakati wizara hiyo pamoja na Idara ya Uhamiaji zikilalamikiwa kutoa vibali vya makazi na kazi kwa wageni bila kuzingatia sheria ambazo zimeainisha bayana kuwa wageni wanaruhusiwa kufanya kazi za kitaalamu tu.

“Ni kweli wapo wengi, lakini hii ni kwa sababu tu ya vyuo wanavyotoka kuwa na utaalamu zaidi, maana huko wanasomea masuala kama uchuaji wa mwili, sidhani kama kwa nchini utaalamu huo upo. Hiyo ndiyo sababu ya kuajiri watu kama hao kutoka nje,” alisema Msaki.

Awali, Msaki alisema kuwa ajira imeongezeka kwa kiwango cha 85,577 sawa na asilimia 6.7 kwa mwaka 2011 kutoka ajira 1,276,982 kwa mwaka 2010 hadi 1,362,559.

Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, takwimu hizo zimeandaliwa na wizara yake sambamba na ofisi ya takwimu ambapo utafiti huo umeonesha kuna ongezeko la ajira za masharti ya muda mrefu 82,969 sawa na asilimia 97 ya ajira zote.

Alisema utafiti umeonesha kuna uwiano kati ya ajira za wanawake ukilinganisha na wanaume, ambapo umeongezeka kufikia asilimia 37.7 ya ajira zote kutoka asilimia 36.5 mwaka 2010 na kwamba idadi ya wanaume imeshuka hadi kufikia asilimia 62.1 ya ajira zote kutoka asilimia 63.5 mwaka 2010.

Katika takwimu hizo, Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza katika kuajiri watu wengi katika sekta rasmi ambapo jumla ya watu 456,815 sawa na asilimia 33.5 kati ya 1,362,559 wameajiriwa.

Kwa mwaka wa fedha 2011/2012 jumla ya ajira 250,678 zilizalishwa kutokana na miradi mbalimbali ya maendeleo ambayo ni pamoja na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) ajira 34,516, Mamlaka ya Maeneo Huru Kiuchumi (EPZA) ajira 15,100 na Kituo cha Taifa cha Uwekezaji (TIC) ajira 82,834.

Je wewe una maoni gani?!

Share this article :

0 comments:

KIKI POLICY


KIKI BLOG POLICY

Blog hii haina lengo la kumdharirisha mtu na pia kutoa taarifa binafsi zenye lengo la kumkwaza mtu,baadhi ya picha na habari katika blog hii hazimilikiwi na KIKI blog bali zinatoka katika vyanzo mbalimbali vya habari. Ikiwa kuna habari au picha yenye kukudharirisha basi usisite kututaharifu mapema hili iondolewe.
KARIBUNI WOTE

BANK WITH DTB 24/7

Blogger Tips and TricksLatest Tips For BloggersBlogger Tricks

WASOMAJI

Receive all updates via Facebook. Just Click the Like Button Below

Powered By Blogger Widgets

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

THIS BLOG IS SPONSORED BY:

KUMBUKUMBU

ZILIZOVUMA

 
----
Support : Copyright © 2015. KIKI NEWS - All Rights Reserved
This blog Designed by and Modified by Joseph Richard